Head image
Govt. Logo

Hits 109579 |  2 online

           


Heshima, nidhamu na uzoefu umepelekea Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya kuonekana inatekeleza majukumu yake.
news phpto

Heshima, nidhamu na uzoefu umepelekea Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya kuonekana inatekeleza majukumu yake na kuleta mabadiliko makubwa kwa watendaji na jamii inayoitumikia.

Heshima, nidhamu na uzoefu umepelekea Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya kuonekana inatekeleza majukumu yake na kuleta mabadiliko makubwa kwa watendaji na jamii inayoitumikia.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt. Saada Mkuya Salum ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume hio Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Kheriyangu Mgeni Khamis kwenye ukumbi wa mkutano Migombani.

Dkt. Saada amesema ujasiri na kujiamini kwake kumepelekea hata watendaji wa Tume kuonekana wapo tayari muda wote kwenye kutekeleza majukumu yao na kufikia malengo kwa mujibu wa majukumu yao ya kazi katika kudhibiti dawa za kulevya, na kupelekea kuiletea heshima nchi yetu kitaifa na kimataifa.

Aidha Dkt Saada amemshukuru bi Kheriyangu kwa utumishi wake na namna alivyoweza kuisimamia taasisi yake pamoja na kuwashughulikia vyema vijana walioachana na matumizi ya dawa za kulevya kuona wanapata nafuu

‘kumtoa mtu katika mazingira hatarishi ya matumizi ya dawa za kulevya na ukamtengeneza akarudi hatika hali yake ya awali na kuanza kuaminiwa na familia na marafiki sio masihara, tumeona ubunifu wa kazi nzuri wanazozifanya huku akizionesha mfano wa kazi hizo’ alisisitiza Dkt Saada.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi Khadija Khamis Rajab amesifu utendaji na jitihada zilizooneshwa na mkurugenzi huyo na kumuomba kuendelea kutoa ushirikiano na ushauri pale panapohitajika .

Akitoa shukurani kwa viongozi wakuu na wakuu wa Taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kitaifa ya Kutaratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Kheriyangu Mgeni Khamis amesema mashirikiano aliyoyapata yamemuwezesha kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Kheriyangu amesisitiza kuwa maamuzi yote aliyokuwa akiyatoa yalikuwa yanapitia kwenye vikao kazi kwa pamoja jambo ambalo limeiwezesha Tume hiyo kupata mafanikio makubwa katika utendaji wa majukumu yake.

Aidha amejifunza mengi ya msingi ikiwemo maisha ya kijamii kwa vile wakati anateuliwa 2013 alikuwa anatokea kwenye jeshi la polisi jambo hili litamsaidia kufahamu namna ya kupambana na wahalifu wakati wa kuendelea na majukumu yake katika jeshi la polisi kwa vile tayari anamtandao mzuri na wanajamii.

Nae Mkurugenzi Mtendaji mpya Luteni Kanal Burhani Nassoro wa Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ameahidi kushirikiana na watendaji na wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuendeleza mazuri yote yaliyoachwa na mtangulizi wake kubuni mbinu mpya katika kusimamia majukumu ya Tume hio.

Akitoa shukurani kwa niaba ya wakurugenzi na wafanyakazi Mkurugenzi Mtendaji Tume ya UKIMWI Zanzibar Dkt. Ahmeid Mohamed Khatib Reja amemshukuru mkurugenzi anaeondoka na kusema kuwa ameacha alama ya upendo na nidhamu iliyodumisha maelewano kwa watendaji na wafanyakazi.

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais imemzawadia cheti cha shukurani pamoja na zawadi nyengine ikiwa ni kuonesha upendo na shukurani kwa muda wote alioitumikia tume hio.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Kheriyangu Mgeni Khamis aliteuliwa mwaka 2013 kuitumikia tume hio hadi April 2021 ambapo anakwenda kuendelea na majukumu mengine ya kazi.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz