Head image
Govt. Logo

Hits 120630 |  2 online

           


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amewataka watendaji wa masuala ya mazingira na mabaraza ya miji kukaa pamoja na ....
news phpto

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya Salum amewataka watendaji wa masuala ya mazingira na mabaraza ya miji kukaa pamoja na kuandaa mpango utakaowawezesha kupata fedha wa kutafuta nyenzo za kufanyia kazi ili mji kuwa katika hali ya usafi

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya Salum amewataka watendaji wa masuala ya mazingira na mabaraza ya miji kukaa pamoja na kuandaa mpango utakaowawezesha kupata fedha wa kutafuta nyenzo za kufanyia kazi ili mji kuwa katika hali ya usafi

Hayo aliyasema wakati alipokutana na watendaji hao pamoja na ujumbe wa watendaji wa Baraza la Jiji juu ya kutafuta namna bora ya kuimarisha usafi wa mji Ofisini kwake Migombani nje kidogo ya mji wa Unguja.

Dkt amesema mbali na hayo ni vyema kuwajengea uwezo wa kitaaluma wahusika ili waweze kufikia malengo yaliokusudiwa ikiwemo kuweka jiji la Zanzibar kuwa safi.

“Ushauri wangu kwenu ni kukaa pamoja baina yenu na watendaji wote wa masuala ya mazingira na watendaji wa mabaraja ya miji ili kuhakikisha wanaandaa mpango ambao utasaidia kupatikana kwa fedha na kutafuta nyenzo za kufanyia kazi,”alisema.

Aidha Waziri Saada alisema upo umuhimu wa wadau hao kufanya kazi kwa pamoja ili kuona maagizo ya viongozi wakuu ya kuweka mazingira safi katika maeneo yote ya miji yanatekelezwa na yanaimarika.

Hivyo katika kufikia hatua hiyo kunahitajika mipango mbali mbali ikiwemo fedha na vitendea kazi stahiki kwa ajili ya kuimarisha eneo kuu la kutupia taka.

Alieleza kwamba bila ya kuwepo kwa mashirikiano kati ya taasisi hizo maendeleo hayatoweza kupatikana na wala mji hautokua safi, hivyo ni vyema kwa taasisi hizo kuzidisha mashirikiano ambayo yatasaidia Jiji la Zanzibar kuwa safi.

Nae Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mstahiki Mahmoud Mohammed Mussa amesema watendaji wa mabaraza hayo wana kila sababu ya kujifunza jinsi ya kuimarisha huduma za usafi wa miji kupitia miji iliyopiga hatua.

Suala la usafi katika Jiji la Zanzibar ni muhimu hasa katika kukuza uchumi kwa vile ni moja kati ya vichocheo vinavyovutia watalii kutoka mataifa mbali mbali kuona mandhari nzuri yenye mazingira safi na salama ya nchi yetu.

“Ni vyema kuiga mfano kwa miji kama Tanga, Arusha na Rwanda kutokana na usafi wa miji yao naamini kama na sisi tufanya hivyo na jiji letu litakua safi watalii wengi kutoka mataifa mbali mbali wataweza kufika kwa wingi na Serikali itakuza uchumi wake,”alisema.

Sambamba na hayo Mstahiki Meya amesema usafi na mazingira ni vitu ambavyo vinakwenda sambamba, hivyo ameziomba taasisi zinazohusiana na usafi kushirikiana na Idara ya Jiji kwani dhamana ya usafi hivi sasa ipo katika ofisi hiyo.

Akizungumzia kuhusiana na hali ya jaa kuu la Kibele liliopo Wilaya ya Kati Unguja, Meneja wa jaa hilo bw Hassan Mohammed Ali amesema kuna haja ya kuimarisha nguvu kazi ya utendaji katika jaa hilo kwani kuna idadi ya wafanyakazi 15 tu.

Alisema jaa hilo lina mahitaji ya wafanyakazi 24 pamoja na kuongeza motisha kwa wafanyakazi kwa kuwapatia posho la mazingira magumu.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz