Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, Dk. Saada Mkuya Salum amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutekeleza vyema majukumu yao ili kufikia lengo lililokusudiwa na Serikali la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, Dk. Saada Mkuya Salum amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutekeleza vyema majukumu yao ili kufikia lengo lililokusudiwa na Serikali la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ameyasema hayo Ofisi kwake Migombani, wakati wa makabidhiano ya Ofisi kwa Makatibu Wakuu, na kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta ufanisi katika utendaji.
Dk. Saada alieleza kuwa, muelekeo wa kazi katika wizara hiyo unakwenda vizuri, hivyo ni vyema kumpa mashirikiano kiongozi huyo, katika kutekeleza majukumu ya Serikali ili kuleta maendeleo.
Aidha amemshukuru katibu anaeondoka kwa mchango wake aliotoa wakati wa utendaji wake, ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza majukumu ya wizara hiyo.
Kwa upande wake aliyekuwa Katibu Mkuu Bi Khadija Khamis Rajab, amesema amepata mashirikiano makubwa wakati wa uongozi na kuwataka wafanyakazi kutoa ushirikiano kwa Katibu Mkuu huyo.
“Katika muda niliofanya kazi katika Wizara hiyo nimeweza kurekebisha mambo mengi kwa mashirikiano niliyoyapata kwa wafanyakazi hivyo nawasisitiza mumpe ushirikiano mkubwa kiongozi mpya”, alisema Bi Khadija.
Nae Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais Dk. Omar Dadi Shajak ameahidi kufanya kazi kwa mashirikiano ili majukumu ya kazi yaendelee ikiwemo uwajibikaji kwa kila mmoja.
“Tushirikiane katika uwajibikaji kwa kila mmoja anapotoka nyumbani akija kazini ajuwe anakuja kufanya kazi zake hadi anapoondoka”, alifahamisha Katibu huyo.
Dk. Shajak aliwataka wafanyakazi hao kuwa wabunifu na kupanga mikakati ya kazi kwa lengo la kukuza ufanisi.