Head image
Govt. Logo

Hits 120668 |  3 online

           


Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia ofisi za viongozi wakuu wa Kitaifa imetoa ushauri kwa Serikali kuhakikisha Kisiwa cha Mnemba kinalindwa
news phpto

Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia ofisi za viongozi wakuu wa Kitaifa imetoa ushauri kwa Serikali kuhakikisha kisiwa cha mnemba kinalindwa, kinaenziwa na kinaendelezwa licha ya kuwa Serikali kupitia ZIPA imetoa utaratibu wa kukodishwa kwa visiwa vidogo vidogo

Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia ofisi za viongozi wakuu wa Kitaifa imetoa ushauri kwa Serikali kuhakikisha Kisiwa cha Mnemba kinalindwa, kinaenziwa na kinaendelezwa licha ya kuwa Serikali kupitia ZIPA imetoa utaratibu wa kukodishwa kwa visiwa vidogo vidogo

Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa Kitaifa Mhe Hassan Hafidh ameyasema hayo walipofanya ziara ya kuangalia maeneo ya hifadhi za mazingira na kushuhudia uharibifu wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na mwanadamu

Mhe Hassan amesema watakaokodishwa visiwa wawe watiifu katika kulinda na kuhifadhi mazingira ya visiwa na kuwasikiliza wataalamu ushauri wanaoutoa kwa kuhakikisha wanaufuata ili kuvilinda visiwa viendelee kuwepo miaka na miaka

Aidha baadhi ya wajumbe nao wameishauri Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuhakikisha maeneo yaliyochimbwa mchanga yanarudi katika uhalisia wake kwa kuotesha miti ya asili ili kuepuka athari zaidi za kimazingira zinazoweza kutokea na kuhatarisha usalama wa maeneo jirani na wanajamii

Nae katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar Dadi Shajak amesema kuna kazi kubwa ya kuhifadhi mazingira kwenye kisiwa cha Mnemba na vyengine vyote vya Unguja na Pemba ili kukuza uchumi wa nchi.

Dkt Shajak amesema pamoja na kukuza uchumi wa nchi pia wanachi wanaozungukwa na kisiwa cha Mnemba nao waweze kunufaika na kuona umuhimu wa uhifadhi wa kisiwa hiki ambacho ni moja kati ya rasilimali muhimu za Zanzibar

“Ni lazima tuweke mazingira ambayo yanakuza uchumi wetu tusibakie tu kuwa tuna rasilimali halafu zimekaa tukaanza kuzivuruga Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inachukuwa nafasi yake katika kuhakikisha elimu inatolewa, mazingira yanahifadhiwa na sheria zinafuatwa katika kila hatua”

Kisiwa cha Mnemba ni miongoni mwa visiwa vidogo ambacho kipo kilomita 3 kutoka usawa wa bahari na Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Unguja chenye ukubwa wa hekta 10.74 ina vuvutio vingi ikiwemo kivutio cha matumbawe ambayo yapo katika eneo la hifadhi ya bahari, kina sifa za kipekee ukilinganisha na visiwa vyengine ambapo asili yake imetokana na uwepo wa fungu mchanga linalozunguka kisiwa chote.

Nae Mkurugenzi wa Hoteli ya Kisiwa cha Mnemba Bw Jonathan Braack amesema mmong’onyoko mkubwa wa fukwe hasa upande wa Mashariki na Kusini ya kisiwa, Uwegeshaji na Utupaji mbaya wa nanga wa boti za kitalii ambao huharibu mwamba na idadi kubwa ya watalii wanaoogelea kwa wakati mmoja ndani ya mwamba wa hifadhi ni changamoto ambazo zinakikabili kisiwa hicho

Jonathan ameelezea baadhi ya hatua zinazochukuliwa kutatua changamoto hizo ikiwemo kuhamasisha upandaji na utunzaji wa miti ya asili katika kisiwa cha Mnemba ili kurudisha uoto wa asili na kuimarisha uhimili wa kisiwa hicho, kutoa elimu na kushirikiana na vijiji jirani katika kukiweka salama kisiwa cha Mnemba na kusaidia miradi kadhaa ya wanajamii

Akielezea kazi zilizopangwa kutekelezwa katika kipindi cha April na Juni 2021 kwa niaba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Saada Mkuya Salum, Dkt Shajak amesema kazi moja wapo ni kufanya mapitio ya sera na sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, kuelimisha jamii masuala yanayohusu UKIMWI na afya ya uzazi.

Kutekeleza shughuli za uratibu na ufatiliaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu, kuteleza shughuli zilizolenga kudhibiti usambazaji,kuuza pamoja na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo kuandaa vikao vya ulinzi na usalama katika Shehia za Unguja na Pemba, kukamilisha maandalizi ya mpango wa muda wa kati wa matumizi ya Bajeti ya Ofisi

Dkt Saada ameendelea kuwakumbusha watumishi wote wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na jamii kwa ujumla kuwa janga la Korona bado lipo na inatupasa kuzingatia miongozo na maelekezo inayotolewa nawataalamu wa afya

Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa imetembelea eneo lilokuwa likitumiwa kuchimbwa mchanga Bumbini Pangatupu na eneo lilikuwa likichimbwa mawe kwa ajili ya ujenzi wa barabara shehia ya Kidaanzini na kisiwa cha Mnemba.

Pia ziara hio itamalizia kwa kutembelea Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Dar es Salaam ili kupata uzoefu kutoka Mamlaka hiyo, Baraza la Taifa la Uhifadhi na usimamizi Mazingira NEMC na kuelekea Kisarawe kwenye mitambo ya kampuni ya Tindwa Medical and Health ya kuchomea taka hatarishi

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz