Head image
Govt. Logo

Hits 120683 |  2 online

           


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amewataka Maafisa Habari wa ofisi hio pamoja na taasisi zilizo chini yake kuwa wabunifu katika utendaji wao wa kazi
news phpto

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar Dadi Shajak amewataka Maafisa Habari wa ofisi hio pamoja na taasisi zilizo chini yake kuwa wabunifu katika utendaji wao wa kazi na kutekeleza majukumu yao ipasavyo

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar Dadi Shajak amewataka Maafisa Habari wa ofisi hio pamoja na taasisi zilizo chini yake kuwa wabunifu katika utendaji wao wa kazi na kutekeleza majukumu yao ipasavyo

Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku ya siku mbili kwa Maafisa Habari na tehama wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na taasisi zilizo chini ya Ofisi hio kwenye ukumbi wa mkutano wa uliopo Migombani, mjini Zanzibar

Dkt Shajak amewakumbusha Maafisa Habari hao kutumia ujuzi wao na kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi na kwa wakati kupitia tovuti, televisheni, redio, magazeti, majarida, mitandao ya kijamii

“Mafunzo haya yanayowalenga nyinyi Maafisa Habari Mawasiliano na Uhusiano muweze kufanya kazi kwa weledi na pia kujitathmini utendaji wenu kwani nina imani baada ya mafunzo haya kutakuwa na mabadiliko katika utendaji wenu wa kazi jambo ambalo litawawezesha wananchi kufahamu majukumu ya Ofisi hii nini tunakifanya, kipi tunakitekeleza na matarajio yetu

Aidha Dkt Shajak amewataka maafisa hao vinara katika kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na OMKR wakielewa kuwa majukumu mahsusi ni Kuratibu masuala ya Uendeshaji, Utumishi na Mipango ya Ofisi, Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa masuala yote ya kisera, mipango ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais

Kusimamia masuala ya Mazingira, Kuratibu na kusimamia masuala ya Ukimwi, Kuratibu masuala ya Udhibiti wa dawa za kulevya, na Kuratibu masuala ya Watu Wenye Ulemavu ili wananchi wafahamu maendeleo yanayofanywa na Serikali yao kupitia OMKR.

”Ili majukumu haya yatekelezwe basi zinazotekeleza sio sera nzuri wala sheria nzuri bali ni utekelezaji wa zile sera na ile sheria yenyewe na wale wanaotekeleza wanahitaji taarifa zao si tu kufika kwa walengwa lakini pia kufika zile taarifa sahihi kwa walengwa na wapelekaji wa taarifa hizo ni nyinyi maafisa habari ”

Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi ndugu Juma Ali Simai amesema maafisa habari hawapaswi kuwa nyuma kutokana na mabadiliko yanayotokea hivyo ni muhimu kupata muda wa kukumbushana na kufahamu mabadiliko ya ulimwengu ili kwenda sambamba na fani yao

Nae Afisa Habari Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Raya Hamad Suleiman kwa niaba ya Maafisa Habari wameahidi kutekeleza vyema majukumu yao kwa kuihabarisha jamii na kutoa ushauri kwani wao ni daraja kati ya Ofisi hio Serikali na wananchi

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz