Maafisa Tehama na wakuu wa vitengo wametakiwa kuwa wabunifu na kushirikiana katika majukumu yao ya kazi ili kuendana na kasi ya iliyopo ya ukuwaji wa teknologia ulimwenguni
Maafisa Tehama na wakuu wa vitengo wametakiwa kuwa wabunifu na kushirikiana katika majukumu yao ya kazi ili kuendana na kasi ya iliyopo ya ukuwaji wa teknologia ulimwenguni
Mkurugenzi Mipango, sera na utafiti Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Bi Daima Mohammed Mkalimoto ameyasema hayo leo wakati akizindua mafunzo kwa maofisa tehama na wakuu wa vitengo wa ofisi hio na taasisi zilizochini yake
Amesema serikali mtandao inatakiwa kuwa hai muda wote katika kutoa ushirikiano ili iwe ni suluhisho la kiutendaji katika mabadiliko na kufanya masuala ya tehama kuwa rahisi na kuwa na mfumo mmoja wenye tija kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Nae mkufunzi wa mafunzo hayo Ndugu Ali Abdi Ali kutoka Serikali Mtandao amesema maafisa tehama ili waendane kasi ya mabadiliko ya mawasiliano ni muhimu wawe wanapatiwa mafunzo ya mara kwa mara jambo ambalo litapelekea kuwa umakini katika utendaji wao wa kazi
Aidha washiriki wa mafunzo hayo waishukuru Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kuomba muendelezo wa mafunzo hayo ili kuwa weledi zaidi na kufahamu maendeleo ya mawasiliano ya tehama, mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Migombani