Head image
Govt. Logo

Hits 120693 |  1 online

           


SERIKALI KUFANYA MAGEUZI YA SERA KUSAIDIA UTUNZAJI WA MAZINGIRA.
news phpto

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema suala la athari za mazingira na mabadiliko ya tabianchi ni la kidunia, ambapo nchi za visiwa zinabaki kuwa waathirika wakubwa, jambo la msingi ni kuweka sera na mipango makini ya kuyalinda.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema suala la athari za mazingira na mabadiliko ya tabianchi ni la kidunia, ambapo nchi za visiwa zinabaki kuwa waathirika wakubwa, jambo la msingi ni kuweka sera na mipango makini ya kuyalinda.

Mheshimiwa Othman ameyasema hayo katika ziara yake ya Wilaya mbili za Mkoa wa Kaskazini Unguja, akiangalia athari za kimazingira zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema pamoja na juhudi mbali mbali zinazosimamiwa na serikali, asasi za kiraia, vikundi vya ushirika na watu binafsi, bado kuna haja ya kufuata mbinu za kitaalamu na njia mbadala za kuyalinda na kuyatunza maeneo, ikizingatiwa kuwa mazingira ni uhai na njia ya maisha ya kila siku, kwa watu kujitafutia riziki.

Mheshimiwa Othman ameeleza azma ya Serikali ya Awamu ya nane kufanya mapitio na marekebisho makubwa ya sera na sheria, yatakayopelekea kuandaa mipango imara ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ili kuyaokoa mazingira, ambayo kwa sasa yanakabiliwa na tishio kubwa la uharibifu sambamba na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mhe Othman, katika ziara yake hiyo ametembelea maeneo mbali mbali yakiwemo ya utunzaji wa misitu chini ya Jumuiya ya Mazingira ya Fujoni (JUMAFU), Shimo la Mchanga la Donge Mchangani, Eneo la Waanika Madagaa la Fungu-Refu, Uendeshaji wa Hoteli ya ZURI unaozingatia utunzaji wa mazingira iliyoko Kijiji cha Kendwa, Majengo yaliyobomolewa na bahari kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi jirani na Soko la Samaki la Nungwi, na Machimbo ya Mawe na Kokoto ya Kandwi, yote katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud, amesema licha ya changamoto katika utunzaji wa mazingira, zikiwemo za ukosefu wa vifaa, nyenzo na ufinyu wa miundombinu, ni vyema kwa wadau kujiunga pamoja ili kunufaika na fursa ambazo serikali imekusudia kuzitoa kwa wananchi kwa utaratibu maalum na mipango ya maendeleo.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu, Bw. Said Juma Ali, amesema juhudi za utunzaji wa mazingira kwa sasa zinakabiliwa na tishio kubwa, kutokana na mabadiliko ya tabianchi baadhi ya watu kugeukia vivutio vya utalii, vikiwemo komba na kima-punju kuwa kitoweleo.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Othman, aliongozana na viongozi mbali mbali wa Kiserikali na wa kijamii akiwemo Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Dkt Omar Dadi Shajak, Mkuu wa Mkoa Kaskazini Mhe Ayoub Mahmoud, Wakuu wa Wilaya za Kaskazini A na B, Ndugu Sadifa Juma Khamis na Ndugu Said Seif, na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na wa Mazingira, Bw. Sheha Mjaja.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz