Head image
Govt. Logo

Hits 111573 |  3 online

           


Dkt Saada Mkuya Salum amewahimiza wananchi na wakulima wa Shehia ya Kiongoni na Mjananza wanasimamia wenyewe mradi wa kujenga tuta
news phpto

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya Salum amewahimiza wananchi na wakulima wa Shehia ya Kiongoni na Mjananza kwenye bonde la Tovuni kuhakikisha wanasimamia wenyewe mradi wa kujenga tuta katika bonde la Tovuni ili uweze kukamilika kwa haraka

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya Salum amewahimiza wananchi na wakulima wa Shehia ya Kiongoni na Mjananza kwenye bonde la Tovuni kuhakikisha wanasimamia wenyewe mradi wa kujenga tuta katika bonde la Tovuni ili uweze kukamilika kwa haraka

Dkt Saada ameyasema hayo wakati akizungumza na wakulima wa bonde la Tovuni na Kiongoni ambapo ameukabidhi mradi huo kwa wananchi ili kazi ya kujenga tuta la kitaalam uanze mara moja kwavile tayari fedha za mradi huo zimeshaingizwa kilichobakia ni utekelezaji

Amesema iwapo wananchi watashirikiana pamoja na kamati walioiunda mradi wa ujenzi wa tuta kwa ajili ya kuzuwia maji ya chumvi yasiingie katika maeneo yao ya ukulima utakamilika kwa muda uliopangwa

“niwaombe sana wananchi na wakulima wa bonde hili kusimama imara kulinda rasilimali zilizopo na kuwa na uchungu wa jitihada zilizochukuliwatutakapo simamia wenyewe mradi huu basi hautafeli na ndio tutakuwa na uchungu wa kulinda eneo hili na rasalimali zilizopo”

Nae Mkuu wa Wilaya ya Wete Bwana Hamad Omar amesifu jitihada zinazochukuliwa na wananchi hao katika kuthamini juhudi zinazochukuliwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ameahidi kuwa fedha ilitolewa mradi huo itatumika kwa lengo lililokusudiwa na utakamilika kwa wakati

Bimkubwa Khamis Omar ambae ni mwanakamati wa bonde hio ametoa shukurani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi kwa kuahidi na kutekeleza kwa vitendo ahadi aliyoitowa wakati wa ziara yake ambapo kwa niaba ya wakulima wenziwe wameahidi kushirikiana na Serikali ili mradi ukamilike kwa wakati

“sasa shida ya kuingiliwa na maji tutakuwa hatunayo tena tuta likishakamilika litatufaa sote hivyo sote ndugu zangu tushikamane isiwe mtu anataka maslahi tu hataki kuja kuwajibika, asiejiweza alete mwanawe au mtu atakaekuwa mbadala wake. Tovuni ni petu tuunganishe nguvu zetu jambo likamilike tufurahie maendeleo tuliyoletewa”alisisitiza Bimkubwa na kushangiriwa na wakulima wenziwe

Aidha sheha wa Shehia ya Kiongoni Bwana Omar Khamis Othman amesema kwa upande wao masheha wote wa Shehia mbili Kiongoni na Mjananza wameahidi kuendelea kutoa mashirikiano kwa wananchi na viongozi kwani mafanikio ni ya watu wote

Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Bi Farhat Mbarouk amesema Mradi wa ujenzi wa tuta la kuzuwia maji ya chumvi yasiingie katika mashamba ya wakulima unagharimiwa na wafadhili kutoka mfuko wa mabadiliko ya tabianchi ambapo fedha zake zinapitia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC

Tayari shilingi milioni 234,702 za kitanzania zimeshaingizwa ili ujenzi huo kuanza mara moja na jumla ya wakulima 271 watafaidika na mradi huo, tuta litakalojengwa litakiuwa na urefu wa mita 450 ambapo wamekabidhiwa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kupitia Idara ya Umwagiliaji kwa vile wao ndio wataalam wa ujenzi huo

Bi Farhat amesema baada ya kukamilika kwa hatua hio mradi huo wakulima hao watapatiwa kazi mbadala ikiwemo ufugaji wa kuku, kufuga samaki na kufuga nyuki

Katika ziara hio ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe DKT Saada Mkuya Salum amefuatana na viongozi wake akiwemo Katibu Mkuu Dkt Omar D. Shajak, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Bw Sheha Mjaja, Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Bi Farhat Mbarouk, Afisa Mdhamin Bw Ahmeid Mbarouk na maafisa wengine

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz