Head image
Govt. Logo

Hits 120687 |  1 online

           


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais awataka watendaji na wafanyakazi wa Ofisi yake kuunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduz
news phpto

Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman ametaka wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini yake kuunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi katika kutekeza majukumu yao ya kiutendaji

Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman ametaka wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini yake kuunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi katika kutekeza majukumu yao ya kiutendaji

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi kwa nyakati tofauti wa Tume ya UKIMWI Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu ambapo amesisitiza suala la nidhamu na uadilifu katika utendaji wao wa kazi na kuwa na mashirikiano ya pamoja ili waweze kujitathmini vyema na kujipima utendaji wao wa kazi

Mhe Harusi amesema kuwa haipendezi kuona wafanyakazi wanabaki ofisini badala yake waende kwa jamii kuwatumikia kwa kutoa elimu hasa skuli, vyuo vikuu na madrasa kwani vishawishi vingi huanzia huko na matokeo yake watoto wadogo wanajiingiza kwenye matendo maovu yakiwemo ya zinaa hatimae kuwepelekea maambukizi ya UKIMWI

“Makosa yakitokezea yanakwenda Serikalini zidisheni juhudi ya mapambano dhidi ya UKIMWI watoto wadogo wanaathirika tu, Taifa hili linatuamini nasi tujiaminishe” alisisitiza Mhe Harusi

Aidha ameagiza kufanyika kwa tathmini ili kufahamu hali halisi ya maradhi ya UKIMWI na kujipanga vyema kuona kipi kinakosekana katika utowaji waelimu ili asilimia iliyopo ya 0.4 isije ikaongezeka na kurudisha nyuma maendeleo na jitihada zilizokwisha kufanyika katika kipindi chote tokea kuingia na kugundulika kwa maradhi ya UKIMWI hapa Zanzibar

Kwa Upande wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu amewataka wafanyakazi wote kufanya kwa mashirikiano bila kujali nani anaulemavu na nani hana na kuisaidia Serikali katika kupanga mipango yake ya maendeleo kwa maendeleo jumuishi

Kwa upande wao wakurugenzi wa Taasisi hizo Mkurugenzi Mtendaji Tume ya UKIMWI Dkt Ahmeid M. Khatib Reja amemuelezea Waziri Harusi kuwa moja kati ya mikakati ya Tume ni kuhakikisha wanaendelea kuyafikia makundi maalum ambayo ndio hatarishi yakiwemo wanawake wanaojiuza miili yao, wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na wanaotumia dawa za kulevya kwa kujidunga sindano

Dkt Ahmeid lengo ni kuwakinga wasiwaathiri wengine “Watu wanaoishi na UKIMWI wataendelea kuwepo ila maabukizi yasikuwepo na ifikapo 2030 tuwe tumemaliza na maambukizi yawe hayapo kama malengo ya dunia yanavyoeleza” aidha amesema Elimu kubwa imetolewa na wanafahamu lakini matendo yao hayaendani na elimu wanayopewa katika mapambano dhidi ya UKIMWI

Nae Mhandisi Ussi amesema baraza linaongozwa na Sheria no 9 ya Watu wenye Ulemavu haki na fursa ya 2006 ambayo kwa sasa inafanyiwa mabadiliko ili iweze kutekelezeka, mpango wa utekelezaji wa sera 2018 na mpango mkakati, ambapo sheria zote zinatokana na mkataba wa Umoja wa Mataifa ambao nchi wanachama wote ikiwemo Tanzania unatakiwa kuufuata

Aidha Mhandisi Ussi pamoja na mambo mengine amesema zipo baadhi ya changamoto ambazo wanazifanyia kazi ikiwemo suala la Watu wenye Ulemavu na afya ya uzazi hasa viziwi wanapokwenda hospitali kujifungua na kupata huduma nyengine za mahitaji ya kiafya

Wakati huo huo Mhe Harusi ametembelea Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo Kanali Burhani Z. Nasoro na kuona hali halisi ya jengo ambalo hali yake imekuwa si ya kuridhisha na linahitaji matengenezo ili waendelee kufanya kazi kwa ufanisi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais tayari ameshatembelea taasisi za Unguja zilizo chini yake na kuzungumza na watendaji wakuu na wafanyakazi, kuangalia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mabadiliko ya tabianchi na kukagua Kituo cha Tiba na Marekebisho ya tabia pamoja na miradi kilichopo Kidimni

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz