Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mh Harusi Said Suleiman amewataka watendaji wa ofisi hiyo kujitathmini na kujipanga upya katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi ili lengo la serikali la utoaji wa huduma bora kwa wananchi liweze kufikiwa kwa wakati
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mh Harusi Said Suleiman amewataka
watendaji wa ofisi hiyo kujitathmini na kujipanga upya katika utekelezaji wa majukumu yao ya
kazi ili lengo la serikali la utoaji wa huduma bora kwa wananchi liweze kufikiwa kwa wakati.
Mh. Harusi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watendaji wa Idara, Tume na Mamlaka
zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais katika mkutano wa kujitambulisha kufuatia
uteuzi wake hivin karibuni ili kuona maendeleo ya taasisi hizo kwenye ukumbi wa mkutano
Gombani Chake Chake.
Amesema ni wajibu wake watendaji na wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na kufuata
muongozo wa utumishi ambapo pamoja na kujitathmini kiutendaji, kuona kipi ambacho
amekifanikisha kwa muda wa wiki nzima ambacho kimeweza kuleta tija kwa taasisi na
wananchi.
Aidha Mh. Harusi amewaambia watendaji hao kuzidisha ari na nguvu ya kiutendaji kwa
wananchi wanaohitaji huduma na kutatua changamoto zao ukizingatia kuwa sekta za ofisi hii ni
mtambuka hivyo hawapaswi kukaa ofisini bali wajitoe kufikisha elimu na huduma stahiki kwa
wanajamii.
“watendaji hakikisheni mnashirikiana pamoja ili wale wanaokufateni mnaowangoza nao waone
kuwa viongozi wao wapo makini na hakutakuwa na mwanya wa kufanya yaliyo sio bali kama
zipo changamoto zigeuke kuwa fursa kwa kuwa wabunifu wa mipango mipya yenye kuleta tija
“alisisitiza Bi Harusi
Mapema Mhe Harusi alionana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mattar Zahor Masoud
na kufanya mazungumzao mafupi ofisini kwake ambapo viongozi hao wote wameahidi
kushirikiana pamoja ili kufanikisha majukumu yatayoleta mafanikio ndani ya mkoa huo kwa vile
masuala yanaosimamiwa na ofisi hio yanamgusa kila mtu.
Afisa Mdhamini wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bw Ahmeid Abubakar amemuahidi
Waziri Bi Harusi kwa kushirikiana na watendaji wanahakikisha wanatekeleza majukumu yao
vyema kusimamia miradi ya maendeleo na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi
Mh.Harusi amezitembelea Idara na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira, Mamlaka ya Kudhibiti
na Kupambana na Dawa za Kulevya, Baraza la Watu wenye Ulemavu na Tume ya UKIMWI pia
ameikaguwa miradi ya maendeleo ukiwemo Mradi wa ujenzi wa tuta la kuzuwia maji ya chumvi
yasiingie katika mashamba uliopo Tovini
Kwengine ni kuona mradi wa ujenzi wa Ukuta wa mawe katika fukwe ya mwambao wa eneo la
Msuka, mradi wa ujenzi wa mabwawa ya maji machafu ulipo Kichungwani, pamoja na kufika
Likoni Kojani kuangalia eneo linalotarajiwa kujengwa ukuta wa kuzuwia mmongonyoko wa
fukwe ambao pia utaunusuru mbuyu wa asili uliopo eneo hilo ambao kwa sasa upo hatarini
kuanguka