Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman amefanya ziara katika taasisi zote zinazosimamiwa na Ofisi yake kwa Unguja na Pemba na kuwataka wafanyakazi kuzingatia misingi ya sheria na kufuata taratibu zote za kazi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman amefanya ziara katika taasisi zote zinazosimamiwa na Ofisi yake kwa Unguja na Pemba na kuwataka wafanyakazi kuzingatia misingi ya sheria na kufuata taratibu zote za kazi katika utekelezaji wa majukumu yao
Mhe Harusi ameyasema hayo kwa nyakati tofauti kwa kuwakumbusha wafanyakazi suala la nidhamu ikiwemo uingiaji na utokaji wa kazini pamoja na kuwataka wakuu wa vitengo kuhakikisha kuwa kila ifikapo mwisho wa mwezi wanaandika taarifa ya utendaji wao wa kazi na kuwasilisha kwa wakuu wao wa kazi
Aidha Mhe Harusi amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi kubakia na mabaibui ofisini na kuwataka wajitofutishe kati wa watoaji wa huduma na wataka huduma “Anakuja mtu anahitaji huduma hajulikani nani anaehudumiwa wala anaehudumia hii haileti picha nzuri” alisisitiza
Amewaagiza wakurugenzi na wasimamizi wa Taasisi hizo kuhakikisha wanasimamia maagizo aliyoyatoa na kufanyiwa kazi kwa kipindi kifupi ili kujenga uwiano kwa wafanyakazi pamoja na kujenga umoja na mshikamano baina yao
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inajukumu la kusimamia masuala mtambuka ambazo ni Idara ya mazingira, Mamlaka ya usimamizi wa mazingira, Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti dawa za kulevya, Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu, Tume ya UKIMWI
Nao wakuu na wasimamizi wa taasisi hizo wameahidi kuendelea kusimamia vyema na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Mhe Harusi ikiwemo kuzidisha mashirikiano ambayo ndio yenye kuleta uhai wa taasisi jambo viongozi wa Ofisi hio wanalisisitiza kwa watendaji na wafanyakazi wote