Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, Agosti 24, 2022, amekutana na Uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira pamoja na Idara ya Mazingira Zanzibar, kwaajili ya kuanza kusimamia utekelezaji wa shughuli za Taasisi hiyo, kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/ 2023.

Kikao hicho ambacho ni muendelezo wa Mhe. Othman, kukutana na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi yake, kimefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza Migombani - Zanzibar, na kuwahusisha pia Viongozi na Watendaji mbali mbali ambao ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza Mhe. Harusi Said Suleiman, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza, Dkt. Omar Dadi Shajak, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Mhe. Sheha Mjaja Juma na Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bi. Farhat Ali Mbarouk.