Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman ameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani katika Viwanja vya Skuli ya Nungwi,Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 01 Disemba 2023
Katika Maadhimisho hayo wanajamii wenye rika tofauti walijitokeza na kupewa huduma za kinga,Elimu ya namna bora ya kujikinga na Maambukizi ya VVU pamoja na Ugawaji wa Vifaa tiba vya kinga na Dawa za kupunguza Maambukizi ya VVU(ARV)
Aidha Taasisi na Mashirika mbali mbali yanayoratibu Masuala ya Afya kama Wizara ya Afya ,UNFPA,AMREF,UNAIDS na UNICEF yameshiriki kutoa huduma na elimu katika Maadhimisho ya siku hii inayoratibiwa na TUME YA UKIMWI ZANZIBAR
Kaulimbiu ya Mwaka huu katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI inasema “JAMII ZIWEZESHE KUONGOZA MAPAMBANO YA UKIMWI”