Head image
Govt. Logo

Hits 109492 |  2 online

           


Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wametakiwa kuendeleza mashirikiano kiutendaji kwa lengo la kutekeleza vyema majukumu malengo na matarajio ya Serikali
news phpto

Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wametakiwa kuendeleza mashirikiano kiutendaji kwa lengo la kutekeleza vyema majukumu malengo na matarajio ya Serikali

Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wametakiwa kuendeleza mashirikiano kiutendaji kwa lengo la kutekeleza vyema majukumu malengo na matarajio ya Serikali kwa kuzingatia maagizo aliyoyatoa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussein Mwinyi

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya ameyasema hayo mara baada ya makabidhiano ya Ofisi hio na aliyekuwa Kaimu Waziri Dkt Khalid Salum Mohamed ambae ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Uratibu wa shughuli za Baraza la Wawakilishi

Serikali ya awamu ya nane inadhamira ya kuondosha kero zinazowakabili wananchi hivyo atahakikisha malengo hayo anayatimiza kwa mashirikiano ya pamoja na wakuu wa Taasisi zote na wafanyakazi katika kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo ya jumla

Dkt Saada amewaomba wafanyakazi kuendelea kumuombea dua aliekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais marehemu Maalim Seif Sharif Hamad aliefariki Febuari 17 mwaka huu ambae aliacha msingi mzuri wa majukumu ya Ofisi hio na jamii kwa ujumla

Akizungumzia changamoto zinazoikabili Ofisi hio Dkt Saada amesema ni muhimu kuangalia mapungufu yaliyopo na kuyapatia ufumbuzi ikiwemo wafanyakazi kupata stahiki zao, kuandaa utaratibu wa kuyalipa madeni pamoja na kuziangalia namna bora ya kuzipitia sheria

‘tuhakikisha tunasimamia stahiki za wafanyakazi ila niwaombe sana wakuu wa taasisi kuwafahamisha wafanyakazi kutofanya kazi kwa mazowea au kupitia migongo ya wengine kwani wapo baadhi ya wafanyakazi hawana ari ya kiutendani hivyo wajiandae maana tunataka kuona vipi mshahara wake anautendea haki kiutendaji’ alisisitiza Dkt Saada

Aidha Mhe Saada amesema Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inasimamia masuala mtambuka hivyo wakuu wa Taasisi wanawajibu wa kusimamia vyema vyanzo vya mapato na kuchangia ukuwaji wa uchumi kama ilivyokusudiwa

Nae Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Uratibu wa shughuli za Baraza la Wawakilishi Dkt Khalid Salum Mohamed ambae alikuwa akikaimu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amewashukuru watendaji na wafanyakazi wote na kuwataka kumpa mashirikiano Mhe Saada ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake

Akitoa shukurani kwa niaba ya watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mkurugenzi kutoka Mamlaka ya Mazingira ndugu Sheha Juma Mjaja wameahidi kumpa mashirikiano na upendo katika utekelezaji wa majukumu ya kazi na kuhakikisha ofisi inakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kuitumikia jamii

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inatekeleza majukumu yake kupitia Ofisi ya faragha, Idara ya mipango Sera na utafiti, Idara ya Uendeshaji na Utumishi , Idara ya mazingira, Idara ya Watu wenye Ulemavu, Mamlaka ya Mazingira, Tume ya Ukimwi, Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya na Afisi Kuu Pemba ambapo inawafanyakazi 306 Unguja na Pemba kati yao 156 wanawake na 150 wanaume .

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz