Head image
Govt. Logo

Hits 81641 |  3 online

           


Marekani yaimarisha mahusiano yake na Zanzibar - Makamu wa kwanza wa Rais
news phpto

Marekani yaimarisha mahusiano yake na Zanzibar - Makamu wa kwanza wa Rais

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema Serikali ya Zanzibar ipo tayari kuendelea kuimarisha mahusiano yake na nchi ya Marekani ili kufikia malengo ya kimaendeleo Zanzibar.

Mheshimiwa Othman, ameyasema hayo mara baada ya kukamilisha mazungumzo na mgeni wake Bwana Donald Wright, balozi wa Marekani nchini Tanzania leo (April 27).

Balozi Donald alifika Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Migombani Unguja, kwalengo la kujitambulisha sambamba na kuimarisha mahusiano mema kati ya nchi hizo mbili.

"Lengo la ujio wetu kwa serikali ya Zanzibar ni kuendelea kuimarisha mahusiano yetu ya muda mrefu, lakini suala la afya, biashara na kutoa elimu kwa wananchi juu ya utumiaji wa fursa zilizopo katika utalii ni miongoni mwa vipaombele vitatu ambavyo tunategemea kuvitekeleza ili kuisaidia Zanzibar" ameeleza Balozi Donald

Nae Makamu wa kwanza wa Rais, alimshukuru Balozi Donald kwa kwaniaba ya nchi ya Marekani kwa namna ambavyo inaendelea kuisaidia Zanzibar.

"Marekani ni nchi rafiki na ina mchango mkubwa kwa Visiwa vyetu vya Zanzibar, kwani itakumbukwa kwamba ilishawahi kutusaidia miradi mbali mbali,kama vile mradi wa kupiga vita malaria, mradi wa umeme pamoja na barabara katika kisiwa cha Pemba ambazo zilikuwa chini ya mradi wa MCC" alifafanua Makamu huyo wa kwanza.

Makamu wa kwanza amemtaka Balozi kuendelea kuitembea Zanzibar, na muda wowote anakaribishwa.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz