Head image
Govt. Logo

Hits 121398 |  6 online

           


SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema inatambua mchango unaotolewa na tasisi za dini hapa Zanzibar katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi
news phpto

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema inatambua mchango unaotolewa na tasisi za dini hapa Zanzibar katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema inatambua mchango unaotolewa na tasisi za dini hapa Zanzibar katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi katika kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kupata elimu hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC) Ahmed Mohammed Khatib alitoa kauli hiyo katika uzinduzi wa machapisho ya uhamasishaji wa wanaumme na watoto kutumia huduma za VVU na Ukimwi kupitia tasisi za kidini Zanzibar katika ukumbi wa Golden Tulip Malindi.

Alisema taasisi za dini zimekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio yaliyofikiwa katika mwitikio wa kitaifa nchini katika kupambana na ugonjwa huo.

Alibainisha kuwa hadi kufikia Disemba 2020, Zanzibar imeweza kufikia malengo ya 90, 90,90 ikiwa 92 kwa 90 ya mwanzo 99 kwa 90 ya pili na 93 kwa 90 ya tatu.

Mkurugenzi Ahmed alisema mafanikio hayo yamepelekea kupunguza maambukizo mapya na vifo vitokanavyo na ukimwi hivyo anaamni kuwa kuna mchango mkubwa wa taasisi za Dini hasa katika kutoa elimu na huduma kwa Jamii kwa haraka na uhakikia

Aidha alisema kwa Zanzibar, takwimu zinaonesha kuwa asilimia 0.4 ya wazanzibari ambao wanaishi na VVU ukilinganisha na asilimia 1 kwa mwaka 2012.

Hata hivyo alibainisha kuwa hadi kufikia Machi mwaka huu kulikuwa na watu 8,147 ambao wanapata huduma katika vituo vya huduma kwa watu wanaoishi na VVU kati yao wanaume 2,526 na wanawake 5,621 na asilimia 4 ni watoto wenye umri wa miaka 14 ni 292.

Alisema pamoja na mafanikio hayo utafiti wa viashiria vya VVU na UKIMWI (THIS) wa mwaka 2016/17 ulionyesha bado kuna maeneo yenye mapungufu yanayotakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka na ushirikikiano wa wadau wote, zikiwemo taasisi za dini. Ikiwemo wanaumme na watoto kuwa nyuma katika upimaji wa VVU, uanzaji wa dawa za ARV na ufuasi endelevu wa dawa hizo.

Alibainisha kuwa takwimu za 2016/2017 zilionesha kuwa asilimia 41 ya wanaume wanaoishi na VVU hawajawahi kupima VVU nchini, hivyo hawajui hali zao lakini wanaojijua wana tatizo la kuanza dawa mapema au kutokunywa dawa hivyo hupelekea kuongezeka vifo vinavyotokana na Ukimwi na VVU.

“Miongoni mwa vifo vinavyojitokeza vingi vinahusisha wanaumme kuanzia umri wa miaka 15 ambao ni 12,000 hufariki kwa mwaka ukilinganisha na wanawake, baadhi ya familia, wazazi wanaoishi na VVU hawajawapima watoto wao walio chini ya miaka 15 na kwa walezi wanaoishi na Watoto wenye maambukizi ya VVU hawajawapeleka Watoto hao kuanza huduma za tiba na matunzo kwa ustawi wao,” alibainisha.

Changamoto nyingine alisema ni kuwepo kwa unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU (WAVIU) hali inayokatisha tamaa baadhi ya wananchi kupima VVU na kuanza huduma za matibabu kwa wakati.

Sambamba na hayo alisema ili kuwafikishia huduma wananchi, serikali kupitia ZAC ina jukumu la kufanya kazi na wadau wote wanaotekeleza afua za VVU na UKIMWI Zanzibar na kutumia Majukwaa mbalimbali kutokana na uwezo walionao katika kuifikia jamii kwa urahisi ikiwemo tasisi za kidini kupeleka habari na ujumbe mpya kwa jamii juu ya huduma za upimaji wa VVU, matibabu mapya na kuibua mijadala inayolenga kuleta mabadiliko chanya ya tabia ili kupunguza maambukizi mapya.

Akitoa salam kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Mkurugenzi Utawala na Rasilimali watu Shekh Othman Mohammed Saleh, alipongeza serikali kupitia tasisi zake ikiwemo ZAC na wizara Afya kwa kushirikiana na tasisi za dini kwani ni muhimu katika kufikisha ujumbe kwa urahisi.

Aidha alisema kushirikiana kwao tokea awali katika kutengeneza machapisho hayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha lengo hilo.

Alisema machapisho hayo yamekuja wakati muafaka hasa kufikia lengo la serikali kumaliza Ukimwi na VVU ifikapo mwaka 2030.

Alisema tasisi za dini ambazo viongozi wake wapo karibu na wananchi katika nyumba za ibada basi wataweza kufikisha elimu hiyo.

"Tunayo nafasi nzuri ya kuhakikisha malengo ya 95 tatu yanafikiwa kwani uwezo tunao kubwa bi kuona tunashiriloana kwa pamoja katika kuhamasisha watu kupima na wale watakaogundulika basi waanze kutumia dawa", alisema.

Nae Msaidizi Meneja wa Kitengo Shirikishi Ukimwi, Homa ya Inni, Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Issa Abeid Mussa, alisema ugomjwa wa Ukimwi hauathiri wanaumme na watoto pekee bali unaathiri watu wengi ulimwenguni.

Aidha alisema elimu hiyo ni vyema kufikia kwa jamii ya kizanzibari na Tanzania kwa ujumla na kuleta matumaini mapya ya kubadilika hali ya mienendo Mila silks na tamaduni zao.

Hata hivyo, aliwapongeza wanawake ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa mstari wa mbele katika kupima VVU.

Hivyo aliomba kusimamiwa jambo hilo kwa dini zote ili kuleta matumaini mapya kwa jamii katika kufikia lengo la serikali kuondoa maambukizi mapya ya VVU.

Michael Lwanda ambae ni mshauri masuala ya Ukimwi na TB kutoka USAID mradi wa Tulonge Afya alisema wameamua kuchapisha machapisho hayo na kushirikisha viongozi wa dini ili kuhamasisha wanaumme na watoto kupata huduma za ukimwi kwani wameonekana kuwa nyuma katika mapambano hayo.

Alisema viongozi wa dini wana nafasi kubwa kutumia misikiti na makanisa kuhamasisha wanaumme na watoto katika maeneo yao waweze kupata huduma za VVU na Ukimwi.

Rev Conon Nuhu Sallanya kutoka Kanisa la Anglican, alisema kila mmoja analazimisha katika mapambano hayo na wasikubali kumrejeshea nyuma hasa kwa waumme ambao wameonekana kuwa nyuma.

“Sasa ni wakati wetu kukusanya nguvu za pamoja kufanya kazi katika jamii kwa kutumia imani za dini zetu na mafundisho yake dini zao ili kuwachukua wanaumme na watoto na kuweza kutembea pamoja katika mapambano haya” alisisitiza.

Hata hivyo alisema anamini wakifanya wajibu wao ipasavyo basi wanawaweza kushajihisha wanaumme na watoto kuweza kutumia huduma hizo.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz