Head image
Govt. Logo

Hits 98054 |  4 online

           


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watu wenye Ulemavu ametowa wito kwa jamii kutoa mashirikiano na Idara ya Watu wenye Ulemavu
news phpto

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watu wenye Ulemavu ndugu Juma Ali Simai ametowa wito kwa jamii kutoa mashirikiano na Idara ya Watu wenye Ulemavu ili kuona wanapata haki sawa na watu wengine wasio walemavu.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watu wenye Ulemavu ndugu Juma Ali Simai ametowa wito kwa jamii kutoa mashirikiano na Idara ya Watu wenye Ulemavu ili kuona wanapata haki sawa na watu wengine wasio walemavu.

Wito huo ameutowa kwa nyakati tofauti wakati alipofanya ziara kutembelea Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu wenye Ulemavu wa akili iliyoko Dole pamoja na kuwatembelea baadhi ya watoto wenye ulemavu kijiji cha Kama, Mtopepo na Meli nne Uzi.

Ndugu Juma amesema si vyema kwa mtu mwenye akili timamu kuwadhihaki kuwabagua na kuwadhalilisha Watu wenye Ulemavu kwa njia yeyote ile bali wanachotakiwa ni kuonesha upendo kwa kuwapa malezi na matunzo.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mfuko wa Uwezeshaji kwa Watu wenye Ulemavu kwa waombaji wa fedha za mfuko huo amewataka kuwa subira kwa vile hivi sasa wanafanya uhakiki na mapitio ili kuwafahamu waliopewa fedha hizo na kuzirudisha kama ilivyo makubaliano yale malengo yake yaweze kufikiwa .

"Tumebaini kuna watu wamepewa fedha za mkopo lakini hawana vigezo na sifa , wapo waliopewa lakini ukiwapigia simu wanasema hawajachukuwa mkopo, wengine tumebaini taratibu za malipo zimekiukwa wakati wa urejeshaji badala kulipa bank lakini wanaona kwenda bank na kupelekea kasi ndogo ya urejeshaji wa fedha za mkopo"

Kutokana na hali hio tayari Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Idara ya Watu wenye Ulemavu inafanya mapitio ya muongozo wa mfuko ili uwendane na hali halisi ya madhumuni ya mfuko wenyewe ili uweze kutoa huduma zaidi ya vile unavyotakiwa

Awali kuliundwa timu ya kutafuta fedha kwa ajili ya mfuko lakini tokea timu imeundwa haijafanya kazi yake ipasavyo ya kuweza kuutunisha mfuko

Mkurugenzi huyo amewahakikishia Watu wenye Ulemavu kuwa Ofisi inashirikiana na maafisa wa mikoa na wilaya katika kufanya uhakiki ili kuwapata wale wote waliopewa fedha za mfuko na uhakiki ukikamilika basi utaratibu utafuatwa kama kawaida kwa vile mfuko umeweka wazi kuhusu uwerejeshaji fedha kwa wale watakaopatiwa mkopo

Nao Watu wenye Ulemavu kutoka maeneo tofauti waliotembelewa wameomba kupatiwa dawa kwa wagonjwa wenye maradhi ya kuanguka, kusaidiwa vyarahani kwa Vikundi vyao ili kujiendeleza kimaisha

Aidha wameomba kuharakishwa kwa uhakiki kwa waliokopeshwa fedha za mfuko ili waanze kupata mkopo na kujiajiri wenyewe

Mkurugenzi Juma amewakabidhi vyarahani viwili Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu wa akili tawi la ZAPDD Dole Wilaya ya Magharibi A, yunifomu za skuli na fedha 50,000 kwa mtoto Tauhida mwenye Ulemavu wa viungo anaeishi Meli nne Uzi

Karibu shilingi mil 160 za mfuko wa Watu wenye Ulemavu zimetolewa na kukopeshwa Watu wenye Ulemavu lakini urudishwaji wake hauridhishi

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz