Head image
Govt. Logo

Hits 109433 |  2 online

           


Makamu wa Kwanza wa Rais amesema ofisi yake itaendelea kuhamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira
news phpto

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema ofisi yake itaendelea kuhamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema ofisi yake itaendelea kuhamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira hasa wa baharini ili kufikia malengo endelevu ya Serikali ya kukuza uchumi.

Mheshimiwa Othman ameyasema hayo leo June 5, katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambapo sherehe za kilele hicho zilifanyika kwa kupanda miti ya mikoko katika eneo la Nyamanzi, ambapo kaulimbiu ni "Tunza mazingira kwa kurejesha uhalisia wake kufikia uchumi wa buluu".

Othman amesema mazingira ni neema kubwa kwetu hivyo ipo haja kubwa kuyatunza na kuyaenzi kwaajili ya maisha yetu. "Kwamujibu wa tafiti za kitaamu, miti aina ya mikoko inauwezo wa kusafisha hewa mara nne zaidi kuliko miti ya kawaida" alieleza.

Aidha Mheshimiwa Othman alitoa wito kwa jamii katika kupanga mikakati endelevu ya kuyarudisha mazingira kuwa sehemu salama, ikiwemo Kuacha tabia ya kukata na kuchoma ovyo miti na misitu,kupunguza matumizi holela ya kuni na mkaa nabadala yake watumie njia mbadala ikiwemo gesi na kulinda na kuhifadhi vivutio vya watalii.

Sambamba na hilo Makamu wa Kwanza wa Rais alitoa zawadi kwa taasisi mbali mbali ambazo zimefanya vyema katika kutunza mazingira, ambapo Hoteli ya Melia,taasisi ya kushajihisha utunzaji wa mazingira na jumuiya ya Uvivu si mtaji ni miongoni mwa waliopata zawadi hizo, sambamba na nakuahidi kuziboresha zaidi zawadi hizo ifikapo mwakani.

Akitoa taarifa ya maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani katibu mkuu wa Wizara ya nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Bi Khadija Khamis Rajab,amemueleza Makamu wa kwanza wa Rais kwamba, kuelekea kilele cha siku ya mazingira duniani idara ya Mazingira iliyopo chini ya ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais imefanya shuguli mbali mbali ikiwemo kuhamasisha kutunza mazingira, kupanda miche ya miti ya mikoko isiyopungua (50,000) katika kisiwa cha Unguja na Pemba pamoja na kusafisha baadhi ya fukwe za bahari.

Akizungumzia eneo ambalo limeharibiwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi huko Nyamanzi, katibu wa Jumuiya ya Ushajihishaji wa mazingira ndugu Iddi Hassan Ali, alisema wanaendelea kulihifadhi eneo hilo, kwalengo la kuanzisha utalii wa kimazingira kutokana na vivutio mbali mbali vilovyopo ambavyo vitapelekea ajira kwa wananchi.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz