Head image
Govt. Logo

Hits 111841 |  2 online

           


Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ametoa wito kwa jamii na watendaji kushirikiana pamoja na Serikali
news phpto

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya Salum ametoa wito kwa jamii na watendaji kushirikiana pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika masuala ya maendeleo na ukuwaji wa uchumi

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya Salum ametoa wito kwa jamii na watendaji kushirikiana pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika masuala ya maendeleo na ukuwaji wa uchumi

Dkt Saada amesema hayo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari ofisini kwake Migombani na kuelezea namna Ofisi yake ilivyojipanga katika kusimamia na kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais

Amesema watendaji wakikaa pamoja kubuni na kupanga, malengo na mikakati ya Serikali itafanikiwa kuelekea mwelekeo sahihi kwa vile katika kujenga lazima kuwe na uchumi shirikishi na endelevu ambao ni wajibu wetu sote

Dkt Saada amesema Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais imefanya Mapitio ya Sera na Sheria ikiwemo za Mazingira, Watu wenye Walemavu na Dawa za kulevya na kufanyiwa marekebisho ambapo rasimu za sheria hizo zipo katika hatua za kuwasilishwa kwa wadau.

Akielezea Uchumi wa Buluu na mikakati ya Ofisi amesema utekelezaji wake inaendana na uchumi shirikishi kwa maana ya kuona wa Watu wenye Ulemavu wanashiriki katika kujenga uchumi wa nchi yao uliobebwa na usimamizi wa mazingira

Uchumi utakaojengwa pia na vijana mahiri kwa maana ya kuwa vijana watakuwa wameepukana na matumizi ya Dawa za Kulevya pamoja na biashara yake, kuondokana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na suala zima la usimamizi na uhifadhi wa mazingira.

Kuhusu suala la Ulemavu Dkt Saada amesema mkakati uliopo ni kupambana na masuala ya yanayosababisha Ulemavu kwa kutumia nyenzo zitazokinga Ulemavu usitokee na kubuni mbinu zitakazopunguza athari zinazosababisha ulemavu

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais itahakikisha inashirikiana vyema na baadhi ya taasisi ikiwemo Wizara ya Afya ili kumsaidia mwananchi kutambua umuhimu wa afya yake na kubuni mbinu na mipango ya kuweza kupunguza ulemavu unaotokana na matatizo ya kiafya

“hili linahitaji mashirikiano zaidi pia na wenzetu wa Jeshi la polisi kutoa elimu kwa wenye vyombo vya moto, baskeli, waendao kwa miguu kufahamu sheria na kingatia alama za barabarani kwa kuepusha ajali za mara kwa mara ambazo zinasababisha ulemavu wa maisha tukiachilia mbali ulemavu wa kuzaliwa.

Dkt Saada ameendelea kuwakumbusha wananchi kuwa UKIMWI bado upo hivyo wasijisahau bali kuchukuwa tahadhari zote za kujikinga na athari za maradhi hayo, kuzingatia miongozo na kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya

Wananchi kujishirikisha katika kazi zinazolenga kuinua uchumi wao na kuacha kijishirikisha na masuala yasio na tija kwa kuiga mambo yasiyo na faida bali ni vyema kufahamu lipi sahihi na lipi si jema kulifanya, utandawazi isiwe kikwazo cha kujiingiza kwenye biashara haramu

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia taasisi zake inaendelea kutoa elimu kwa jamii katika masuala yote mtambuka ambayo yanawagusa Watu wenye Ulemavu, Usimamizi wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, Kuratibu Muitiko wa Taifa wa Ukimwi na Udhibiti wa Dawa za Kulevya

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz