Head image
Govt. Logo

Hits 112694 |  5 online

           


Katibu kuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amesema uwepo wa sera na sheria zinazoendana kati ya Tanzania bara na Zanzibar ni fursa ya kuongeza ufanisi na kufikia malengo ya taasisi hizo
news phpto

Katibu kuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar Dadi Shajak amesema uwepo wa sera na sheria zinazoendana kati ya Tanzania bara na Zanzibar ni fursa ya kuongeza ufanisi na kufikia malengo ya taasisi hizo

Katibu kuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar Dadi Shajak amesema uwepo wa sera na sheria zinazoendana kati ya Tanzania bara na Zanzibar ni fursa ya kuongeza ufanisi na kufikia malengo ya taasisi hizo

Ameyasema hayo katika kikao cha mashauriano ya pamoja kati ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu na ujumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wenye lengo la kukuza ushirikiano na kubadilishana uzoefu hasa katika sekta ya Watu

wenye Ulemavu.

Dkt Shajak amesema katika kukuza ufanisi ni vyema kuimarisha uhusiano wa karibu uliokuwepo wa taasisi zote mbili kuzungumza lugha moja ya kiutendaji kwa vile kila upande una mafanikio na changamoto za kiutendaji lakini mwisho wa siku tunazungumzia mafanikio na maslahi ya Watanzania ya Watu wenye Ulemavu.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Adam amesema lengo la ujio wao ni kujifunza kutoka pande zote mbili kwa kubadilishana uzowefu na kuangalia miongozo wapi panahitaji maboresho pamoja na kupeana mawazo ya kiutendaji

“leo tumejifunza utaratibu mzuri uliopo wa kukusanya takwimu za Watu wenye Ulemavu ambazo zinakwenda mpaka kwenye Shehia hili tunaondoka nalo na wenzetu wa Zanzibar tumeona wao bado hawajawa na vyuo katika stadi za kazi na marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu hapa tunaona kuwa tumepata kitu kizuri kwa pande zote mbili na tutafanya kazi kwa pamoja “alisisitiza Profesa Jamal

Mkurugenzi wa Baraza la taifa la Tatu la Watu wenye Ulemavu ndugu Ussi Khamis Debe amesema Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu na Sekretarieti yake wanashughuli kubwa ya kuratibu masuala ya Watu wenye Ulemavu kwa Serikali na kijamii kwa ujumla

Nae Mkurugenzi anaeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ndugu Jacob Mwinula amesifu uwepo wa mfumo wa kielekroniki ambao unarahisisha kupata taaarifa sahihi kwa ajili ya ustawi wa haki za watu wenye ulemavu, pamoja na suala la miundo mbinu ambapo amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa hivyo watahakikisha miongozo hio wanaifanyia kazi kwa manufaa ya kiutendaji

Aidha Jacob amesema Watu wenye Ulemavu wanayo haki na nafasi ya kujiendeleza na kupata huduma kwa jamii sawa na watu wasio na ulemavu na kuongeza kuwa ushiriki wao katika maisha ya kila siku ndani ya jamii hauna budi kulenga katika kupunguza au kuondosha maisha tegemezi

Katika kikao hicho mapendekezo kadhaa yametolewa ya kukuza ushirikiano ikiwemo kuwepo ushiriki wa pamoja kati ya Zanzibar na Tanzania Bara kwenye ushiriki wa mikutano ya kimataifa na kikanda

Kuimarishwa mashirikiano juu ya utekelezaji wa mikataba ya kimataifa juu ya haki za Watu wenye Ulemavu pamoja na kuangaliwa suala la Watu wenye Ulemavu kama ni suala la haki za kibinaadamu Tanzania nzima

Vikao hivyo ni muendelezo wa mikakati ya serikali katika kuimarisha

utendaji kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa sekta ya Watu wenye Ulemavu.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz