Head image
Govt. Logo

Hits 116058 |  1 online

           


Watu wenye Ulemavu wana haki ya kushirikishwa katika nyanja zote za kiuchumi kama raia wengine
news phpto

Watu wenye Ulemavu wana haki ya kushirikishwa katika nyanja zote za kiuchumi kama raia wengine wote wa nchi hii bila ya kujali ulemavu wao kwani kinachoangaliwa si ulemavu wao bali ni haki zao na uwezo walionao

Watu wenye Ulemavu wana haki ya kushirikishwa katika nyanja zote za kiuchumi kama raia wengine wote wa nchi hii bila ya kujali ulemavu wao kwani kinachoangaliwa si ulemavu wao bali ni haki zao na uwezo walionao

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Bi Salma Saadat Haji ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu ambayo huadhimishwa kila ifikapo Disemba 3 ya kila mwaka kwenye ukumbi wa Baraza hilo uliopo Migombani

Bi Salma amesema haki ya kushiriki katika harakati za maendeleo imeelezwa kwenye Ibara ya 29 ya Mkataba wa Kimataifa wa Watu wenye Ulemavu ulioridhiwa na Tanzania mwaka 2009,

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeweka muongozo maalum ili maendeleo ya nchi yasiwaache nyuma Watu wenye Ulemavu kwa kuboresha muundo wa taasisi ya Watu wenye Ulemavu

Maboresho hayo ni pamoja na kuanzisha Maafisa Walemavu Mkoa, Wilaya na Kamati za Shehia jambo linalorahisisha kuibua changamoto mbali mbali za Watu wenye Ulemavu kuanzia ngazi ya Shehia na Serikali kuzifanyia kazi kwa haraka changamoto hizo.

Nae Mkurugenzi Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Mhandisi Ussy Khamis Debe amesema kuna mafaniko mengi yaliyopatikana tokea ilipokuwa Idara hadi Baraza ikiwemo kuwa na takwimu za Watu wenye Ulemavu kupitia usajili na mfumo wa Kielektroniki unaojulikana kama Mfumo Jumuishi

Injinia Ussy amesema kuwepo kwa mpango mkakati wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu (2019 – 2024) utasaidia Baraza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuishauri Serikali hatimae kutekeleza vyema masuala muhimu ya Watu wenye Ulemavu

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu katika kuimarisha zaidi usimamizi wa fursa na haki za Watu wenye Ulemavu, imefanya mapitio ya awali ya Sheria ya Watu wenye Ulemavu (Haki na Fursa) No.9 2006 ambapo rasimu yake inaendelea kupata maoni ya wadau ambapo marekebisho ya sheria hii yataongeza ufanisi katika utoaji wa haki na fursa kwa Watu wenye Ulemavu

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Uongozi na Ushirikishwaji Watu wenye Ulemavu, kuelekea Ujumuishwaji na Ufikiwaji endelevu baada ya UVIKO 19 Duniani” ambapo kwa mwaka huu maadhimisho ya siku ya Kitaifa kwa Watu wenye Ulemavu yatafanyika Disemba 4 kwenye kiwanja cha Hamburu Kijiji cha Nungwi kilichoko kwenye Mkoa wa Kaskazini Unguja, Wilaya ya Kaskazini “A”

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz