Head image
Govt. Logo

Hits 120656 |  3 online

           


Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea shamra shamra za sherehe za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar
news phpto

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema katika kutekeleza azma ya serikali juu ya kudhibiti uingizaji na matumizi ya dawa za kulevya hatua zimechukuliwa kadhaa zimechukuliwa ikiwemo kufuta sheria iliyokuwepo awali

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema katika kutekeleza azma ya serikali juu ya kudhibiti uingizaji na matumizi ya dawa za kulevya hatua zimechukuliwa kadhaa zimechukuliwa ikiwemo kufuta sheria iliyokuwepo awali

Amesema sheria iliyofutwa ni ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya (Namba 9/2009) na kutunga sheria mpya itakayopelekea kuunda Mamlaka itakayokuwa na nguvu za kisheria za kupambana na dawa za kulevya

Dkt Saada ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea shamra shamra za sherehe za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni.

“Ili kuimarisha mapambano ya wimbi la uingizaji, ulimaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo kupitishwa kwa Mswaada wa Sheria ya Marekebisho ya kuanzisha Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya”

Amesisitiza kuwa Mamlaka hio itakayokuwa na uwezo wa kupeleleza, kukamata, kuchunguza na hatimae kupeleka Mahakamani mashauri yanayohusiana na dawa za kulevya pamoja na makosa mengine yanayofanana nayo.

Akizungumzia maendeleo katika sekta ya mazingira kwa kipindi cha miaka 58 amesema Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais kupitia Idara na Mamlaka ya usimamizi wa Mazingira inakusudia kufanya uhakiki katika maeneo yote ambayo yameathiriwa na mabadiliko ya tabia yanchi na shughuli za zinazotokana na binaadamu

Hatua hio itasaidia kufahamu hatua za kuchukuliwa pindipo inapotokezea athari na kutolea mfano wa maeneo yanayohitaji kupandwa miti kwa kufahamu aina miti inayohitajika kwa mujibu wa eneo husika,

Aidha amesema kwa sasa tayari wamerejesha maeneo kadhaa kwa Unguja na Pemba yalioathiriwa kutokana na mmong’onyoko wa fukwe na uingiaji wa maji ya chumvi katika maeneo ya kilimo na makaazi, athari ambazo zimesababishwa na mabadiliko ya tabianchi

Kwa upande wa Tume ya UKIMWI, Dkt Saada amesema imeongeza hamasa ya upimaji wa hiari hususan kwa vijana pamoja na kuendelea kuzuia maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Tume ya UKIMWI inaendelea kutoa elimu na kuhakikisha kuwa jamii inaongeza uelewa juu ya masuala mbali mbali yanayohusu UKIMWI ili kuisaidia jamii kujiepusha na tabia hatarishi zinazochangia kasi ya maambukuzi ya virusi vya maradhi ya UKIMWI

Akizungumzia kuhusu Watu wenye Ulemavu amesema Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu na Sekretarieti yake wanashughuli kubwa ya kuratibu masuala ya Watu wenye Ulemavu katika serikali na kijamii kwa ujumla.

Kulingana na muongozo wa miundombinu rafiki kwa Watu wenye Ulemavu uliotolewa na Serikali, kumekuwa na marekebisho ya miundombinu kadhaa ambayo yameendelea kufanyika katika majengo hususan ya Serikali. (tuyataje ikiwezekana).

Dkt Saada amesisitiza kuwa Serikali imechukua hatua za makusudi kuimarisha njia za watembea kwa miguu katika barabara kuu walkways), ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kwa Watu wenye Ulemavu kupunguza vihatarishi vilivyokuwa vikitokea hapo awali na kuwaongezea usalama zaidi wanapozifuata huduma mbalimbali.

Mwisho Dkt Saada ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kuzidisha mshikamano ili kuenda sambamba na ukuwaji wa uchumi na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika masuala mtambuka yanayohusu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inatarajia kuwa na jamii inayoishi katika Mazingira endelevu, iliyohuru na matumizi ya Dawa za Kulevya, UKIMWI na inayofurahia Haki na Fursa za Watu wenye Ulemavu, kwa ajili ya kufikia Uchumi endelevu kwa faida ya wananchi wa Zanzibar.

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inatoa pongezi na kumtakia kheri Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na Wazanzibari wote kuelekea maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Zanzibar

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz