Head image
Govt. Logo

Hits 120690 |  1 online

           


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amesema mara baada ya Mapinduzi, tarehe 23/9/1964 Serikali ya ilitangaza elimu bila malipo kwa wazanzibari wote
news phpto

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya Salum amesema mara baada ya Mapinduzi, tarehe 23/9/1964 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilitangaza elimu bila malipo kwa wazanzibari wote bila ya kujadi rangi zao, dini zao, itikadi zao na asili yao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya Salum amesema mara baada ya Mapinduzi tarehe 23/09/1964 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilitangaza elimu bila malipo kwa wazanzibari wote bila ya kujadi rangi zao, dini zao, itikadi zao na asili yao.

Amesema ieleweke kuwa tangazo la elimu bila malipo lilikuwa na maana ya kuongeza fursa za kupata elimu iliyo bora kwa wote itakayomuwezesha Mzanzibari kukabiliana na changamoto mbalimbali katika Maisha yake kwa faida yake mwenyewe, wazazi na taifa kwa ujumla.

Dkt Saada ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua Jengo la Madarasa manne Skuli ya Maandalizi na Msingi ya Binguni, Wilaya ya Kati ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

Ameema ujenzi wa Jengo la skuli ya Binguni ni kielelezo tosha cha juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha nafasi za masomo kwa watoto wote zinapatikana katika maeneo yote ya nchi yetu.

“viongozi wa Mkoa wa Kusini wanahakikisha hawaachwi nyuma katika mkoa huu hasa katika suala la elimu na kukuwa kiwango chake, Binguni lazima iwe inaongoza na ninaimani mtafanikiwa kuongoza kwa ari kwa sababu uwezo upo mazingira mazuri yapo hakuna sababu ya wanafunzi kufeli wazazi tushirikiane” alisisitiza

Aidha Dkt Saada ametoa wito kwa wazee, wanafunzi na jamii kwa ujumla, kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuitunza skuli hii yakiwemo majengo na vifaa vyote pamoja na kuwaomba kupanda miti na bustani za aina mbalimbali katika maeneo ya skuli ili kuimarisha mazingira ya skuli.

Amewahimiza wazazi kuzifuatilia nyendo za watoto, kufuatilia maendeleo yao ya masomo na pia nidhamu zao pamoja na kuhakikisha kuwa hawajishirikishi na mambo maovu na wanakuwa salama wakati wote ili kuepukana na vitendo vya udhalilishaji.

Mhe Dkt Saada ametoa shukurani za dhati kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kumpa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika shughuli ya ufunguzi wa mabanda hayo viongozi, pamoja na wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika sherehe hio

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Bwana Ali Khamis Juma amesema katika kutekeleza dhamira ya Mapinduzi ya kuwapatia wazanzibari wote elimu bila ya malipo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 1964 iliweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha utekelezaji wa tamko la elimu bila malipo linafanikiwa

Miongoni mwa mikakati hiyo ni kuimarisha miundombinu ya elimu ili kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anayekosa nafasi ya kujipatia elimu popote alipo ambapo amesema kabla ya Mapinduzi, Zanzibar ilikuwa na skuli 62 tu za msingi.

Hadi kufikia mwaka 2021 idadi ya skuli imeongezeka na kufikia skuli 545 zinazotoa elimu ya msingi zenye jumla ya wanafunzi 331,425 Unguja na Pemba, ujenzi wa Jengo la Madarasa manne Skuli ya Maandalizi na Msingi ya Binguni umegharimu zaidi ya shilingi milioni 31

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Mhe Hadidi Rashid, Mkuu wa Wilaya Kusini na Wilaya ya Kati, wakurugenzi kutoka Wizara ya Elimu na maafisa tawala, Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu na Mbunge wa Kwahani, viongozi wengine wa chama pamoja na wananchi.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz