Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt. Saada Mkuya Salum, alisema wananchi wamekuwa na mwamko mkubwa wa kutunza na kuhifadhi mazingira kwa vile wamefahamu kuwa ni njia moja wapo ya kuwasaidia kujiinua Kiuchumi kupitia uhifadhi wa mazingira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt. Saada Mkuya Salum, alisema wananchi wamekuwa na mwamko mkubwa wa kutunza na kuhifadhi mazingira kwa vile wamefahamu kuwa ni njia moja wapo ya kuwasaidia kujiinua Kiuchumi kupitia uhifadhi wa mazingira.
Ameeleza hayo katika ziara ya kutembelea maeneo ya mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia ekolojia (EBA) na kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Matemwe Shehia ya Kijini, Mbuyutende na Jugakuu Wadi ya Kijini Mkoa wa Kaskazini Unguja.akiwa na Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Said Jaffo na viongozi wengine alioambatana nao
Kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Uhimili wa Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia mfumo ikolojia vijijini Dkt Saada ameshauriana na Waziri Jaffo kuangalia uwezekano wa kuanzisha miradi mengine itakayosaidia sekta nyengine ya ardhini inayohusisha mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
"Mazingira ndio uchumi tumieni mazingira yaliyowazunguka kwani hivi sasa imeonekanwa wananchi wamekuwa wakikuza uchumi wao na kipato chao kimekuwa kikiongezeka kwa kasi ya ajabu kwa kutumia miti kutengenezea bidhaa mbalimbali na kuuza kwa wageni na wenyeji" alisema.
Dkt Saada amesema lengo la mradi huu ni kusaidia kuhimili mabadiliko ya ya tabianchi, kwa kurejesha uoto wa asili kwa kutumia mfuko wa ikolojia, kutoa elimujuu ya kilimochenye kustahamiliathari za mabadiliko ya tabianchi na kuwangea uwezo wanajamiijuu ya njia mbadala za kujipatia kipatoambacho hakiathiri mazingira
Nae Waziri wa Nchi, Afisi ya Raisi, Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Jaffo, amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutafuta njia mbadala za utunzaji na uhifadhi wa mazingira hasa katika maeneo ya fukwe ambayo yanaharibiwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
Waziri Jaffo, alisema katika mradi wa EBA amefarijika kuona mradi huo unaendelea kutoa manufaa kwa jamii ambapo umekuwa ukiwasaidia wananchi katika kujipatia ajira hasa kinamama na vijana wamekuwa wakijishughulisha katika kujikwamua kiuchumi.
Hivyo, aliwataka wananchi kuacha matumizi mabaya ya Misitu na uharibifu wa mazingira kwa lengo la kuona hali ya mazingira inaendelea kuwa imara na bora zaidi ili kuweza kuwanufaisha wananchi ambao wamekuwa wakitumia kwa matumizi mbalimbali.
Akizungumzia athari zinazosababishwa na uharibifu wa mazingira Dkt. Jaffo alisema kuwa kwa sasa maeneo mengi yakiwemo Zanzibar hasa ya fukwe yamepata athari za uharibifu wa mazingira kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi, hivyo alisema ni vyema wananchi kuendelea kutunza mazingira ili uharibifu upungue na athari zisiendelee kutokea.
Pamoja na hayo, alisema kuwa lengo la mradi huo ni kusaidia kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kurejesha uoto wa asili kwa kutumia mfuko wa ikolojia, kutoa elimu ya juu ya kilimo chenye kustahamili athari za mabadiliko ya tabianchi sambamba na kujengea uwezo wanajamii juu ya njia mbadala za kujipatia kipato ambacho hakiathiri mazingira.
Sambamba na hayo, Dkt Jaffo alisema kuwa kupitia mradi huo jumla ya dola za kimarekani 17,413,835, 900 ambao kwa upande wa Zanzibar jumla ya shilingi 1,100,112,000 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.
Hata hivyo, aliwataka watendaji waliopewa kazi ya kuchimba visima kupitia mradi huo kumaliza kazi zao kwa mujibu wa makubaliano kabla ya mwaka wa fedha 2021-2022 haujakamilika kuweza kukamilisha kazi hiyo ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama.
Eneo jengine walilotembelea ni kuangalia na kupata maelezo ya kazi za vikundi vya utengenezaji sabuni na vipodozi visivyotumia kemikali ikiwemo liwa, mafuta ya kujipaka kwa kutumia majani ya mchaichai, mkaratusi, karafuu na miti mengine ya asili kutoka kwa Bi Fatma Omar Juma wa Kikundi cha utengenezaji wa sabuni na vipodozi Matemwe Kijini na nyumba ya Bi Tatu Zaja Haji kuona jiko sanifu la kuni kidogo
Wakati huo huo Mawaziri hao wanaoshughulikia masuala ya mazingira wametembelea eneo la fukwe ya Nungwi ambayo imeathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi na kuta zake kuanguka ikiwemo baadhi ya hoteli, madrasa na nyumba za wananchi na kwa pamoja wameahidi kukaa pamoja na kushughulikia suala hilo
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Ayoub Mohamed Mahmoud, ameahidi kuwa uongozi wa Mkoa wa Kaskazini utasimamia vyema miradi ya maendeleo iliyopo na ile ambayo haijakamilika iweze kutekelezwa kwa wakati.
Mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia ekolojia umefadhiliwa na mfuko wa mazingira wa kimataifa (GEF) na Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ambapo umeweza kuwajengea uwezo wajasiriamali, kuanzisha kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, na kuandaa mpango wa usimamizi wa matumizi ya ardhi.
Mradi wa EBA ni wa miaka mitano unatekelezwa ndani ya Mikoa mitano kwenye Wilaya tano ambapo kwa upande wa Tanzania Bara ipo kwenye mikoa minne ikiwemo Wilaya ya Simanjiro, Wilaya ya Kishapu, Wilaya ya Mpwapwana Wilaya ya Mvumero na kwa Zanzibar ni Mkoa wa Kaskazini ndani ya Wilaya ya Kaskazini “A” katika Shehia za Matemwe Kijini, Mbuyutende, na Jukakuu Wadi wa Kijini.