Head image
Govt. Logo

Hits 120635 |  3 online

           


Kuanzishwa kwa mamlaka ya udhibiti na kupambana na dawa za kulevya Zanzibar kutaongeza kasi ya mapamano dhidi ya dawa za kulevya hapa nchini.
news phpto

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeleza kuwa kuanzishwa kwa mamlaka ya udhibiti na kupambana na dawa za kulevya Zanzibar kutaongeza kasi ya mapamano dhidi ya dawa za kulevya hapa nchini.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeleza kuwa kuanzishwa kwa mamlaka ya udhibiti na kupambana na dawa za kulevya Zanzibar kutaongeza kasi ya mapamano dhidi ya dawa za kulevya hapa nchini.

Mamaaka hiyo iliyoanzishwa chini ya sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar, Namba 8 ya mwaka 2021 inaipa nguvu zaidi mamaka hiyo kuliko ilivyokuwa awali kwa tume ya taifa ya kuratibu na udhibiti wa dawa za kulevya iliyokuwa ikifanya kazi ya uratibu na udhibiti wa dawa hizo.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Dk Saada Mkuya Salum, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo Migombani, wilaya ya Mjini Unguja.

Alisema hatua iyo itaifanya mamlaka hiyo kuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu yake juu ya kupambana na uraibu uwo ambao kwa kiasi kikubwa unachangia kuharibu vijana na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

“Hatua iyo imeipa uwezo kamili mamlaka iyo kupeleleza, kukamata, kuchunguza na hatimae kupeleka Mahkamani mashauri yanayohusiana na dawa za kulevya pamoja na makosa mengine yanayofana na hayo,”alisema.

Sambamba na hayo alisema hatua hiyo itaifanya mamlaka hiyo kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi pamoja na kuifanya Zanzibar kuwa salama katika kuathiriwa na matumizi ya dawa izo.

Alisema chombo icho kitaongozwa na Kamishna mkuu ambacho kitakuwa chini ya Baraza la Taifa la kudhibitii na kupambana na dawa za kulevya litaloongozwa na Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Hata hivyo alifahamisha kwamba sheria hiyo imeweza kumpa nguvu kubwa Kamishna mkuu wa taasisi hiyo kwa kuweza kukagua, kuweka kizuizini na kufanya uchunguzi kuhusiana na makosa yaliyochini ya sheria hii.

Aidha alifahamisha kwamba sheria hiyo pia imeweza kutoa majukumu kwa taasisi za umma katika kujumuika pamoja juu ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya hapa nchini.

“Ni vyema jamii kujiepusha na shughuli mbalimbali zinazohusiana na bidhaa hiyo ikiwemo kufadili biashara hiyo, kujihusisha kwa namna yoyote ikiwemo kuzalisha,kutumia na hata kufanya kazi nyengine yeyote ukibainika basi adhabu yake ni kifungo cha maisha na kutaifishwa mali zote,”alisema.

Mbali na hayo alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kujiepusha kujiingiza katika uhalifu huyo kwani utasababisha kuwaletea athari kubwa kutokana na sheria iliyopo hivi sasa kali na inawabana watu wote kwa namna moja au nyengine endapo utajihusisha na shughuli za dawa za kulevya.

Kamishina wa mamlaka ya kuthibiti na kupambana na madawa ya kulevya Zanzibar Nassor Burhan, alisema kupitia sheria hiyo imesaidia kuwepo kwa mahakama maalum na mahakimu maalum wa kushulika na kesi hizo kwa urahisi na ufanisi.

Alisema hivyo taasisi hiyo imejipanga vizuri katika kutekeleza majukumu yake kwani wamejipanga kufatila kesi zote zitakazowalishwa za dawa za kulevya na kuziwekea umakini juu ya kufanyia upelelezi ndani ya saa 24 au 48 ili kuchochea uendeshaji wa kesi izo.

“Mahakama kwa ajili ya madawa ya kulevya na kuhakikisha kesi zote zitachunguzwa ndani ya masaa hayo na kesi kuendeshwa ndani ya wiki moja itakuwa imekamilika,”alisema.

Sambamba na hayo aliomba wananchi wote kushirikiana na jeshi la polisi hasa mzazi au mlezi ilikupinga vitendo hivyo vibaya vya dawa za kulevya.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz