Head image
Govt. Logo

Hits 109438 |  1 online

           


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango amewataka Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuendelea kuwa wabunifu ili kwenda sambamba na maono ya Serikali ya awamu ya nane
news phpto

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dk. Saada Mkuya Salumu , amewataka Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar kuendelea kuwa wabunifu ili kwenda sambamba na maono ya Serikali ya awamu ya nane ya kutimiza matarajio ya kuwatumikia vyema wananchi.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dk. Saada Mkuya Salumu , amewataka Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar kuendelea kuwa wabunifu ili kwenda sambamba na maono ya Serikali ya awamu ya nane ya kutimiza matarajio ya kuwatumikia vyema wananchi.

Mhe. Mkuya ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya ofisi baina yake na Waziri mpya wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe, Harusi Said Suleiman kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri Zanzibar yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi hivi karibuni.

Amesema kwamba wananchi wanamatarajio makubwa ya Serikali ya awamu ya nane katika utekelezaji wa sera na mipango mbali mbali ya maendeleo na kwamba ni vyema wafanyakazi kujitahidi kwenda sambamba na matarajio hayo ya serikali.

Hata hivyo, amewakumbusha watendaji hao pia kujitahidi kuendelea kwenda sambamba na muda wakati utekelezaji wa shughuli zao mbali mbali ili kumsaidia waziri Harusi kutimiza vyema majukumu yake.

Amehimiza wafanyakazi hao kumpa mashirikiano Waziri Harusi kama walivyompa yeye ili aweze kutumiza majukumu yake kwa wepesi na kuweza kupata mafanikio katika sekta zote mtambuka anazoziongoza ndani ya wizara hiyo.

Naye waziri mpya wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Harusi Said Suleiman, amewaomba wafanyakazi hao kumpa mashirikiano katika kufanikisha utekelezaji wa shughuli za wizara na ujenzi wa nchi kwa jumla.

Aidha amewakumbusha watendaji hao umuhimu wa kuendelea kufanyakazi kwa mashirikiano na kuheshimu sheria na taratibu za kazi kama msingi wa mafanikio kazini.

Aidha amezitaka taasisi zote za ndani kuhakikisha kwamba zinatayarisha na kutekeleza mpango mkakati katika utekelezaji wa malengo ya taasizi husika.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dk. Omar D. Shajak, amemshukuru waziri aliyeondoka Mhe. Dkt

Saada Mkuya kwa usimamizi bora kwa kipindi chote alichokuwepo kwa kutumia umahiri na maono mapana katika kusimamia sekta zilizopo ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.

Dkt Shajak amesema kwamba katika kipindi kifupi alichoiingoza Ofisi hiyo usimamizi wake umeweza kusaidia sana ofisi hiyo kutekeleza mambo mengi kwa ufanisi mkubwa likiwemo suala la mabadiliko ya sheria ya kupambana na dawa ya kulevya Zanzibar.

Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Migombani

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz