Head image
Govt. Logo

Hits 131644 |  1 online

           


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amesema lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kutoa fursa na haki kwa Watu wenye Ulemavu na kuhakikisha kunakuwa na maendeleo jumuishi
news phpto

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar D. Shajak amesema lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kutoa fursa na haki kwa Watu wenye Ulemavu na kuhakikisha kunakuwa na maendeleo jumuishi yanayozingatia mahitaji ya watu wote na kuzingatia mahitaji Watu wenye Ulemavu

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar D. Shajak amesema lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kutoa fursa na haki kwa Watu wenye Ulemavu na kuhakikisha kunakuwa na maendeleo jumuishi yanayozingatia mahitaji ya watu wote na kuzingatia mahitaji Watu wenye Ulemavu

Ameyasema hayo kwenye mafunzo ya maendeleo jumuishi kwa Wakurugenzi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwemo wakurugenzi Uendeshaji na Utumishi pamoja na Wakurugenzi Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara na taasisi za Serikali kwenye ukumbi wa mkutano wa Hoteli ya Madinatul Bahri

Dkt Shajak ameeleza kuwa umuhimu wa mafunzo hayo kupewa wakurugenzi kwa vile wao ndio moja kati ya kiini katika kila wizara kwa vile wao ndio waratibu watengeza sera, waendeshaji na ndio wanaozalisha mipango ya serikali, wanaotengeneza sera na kusimamia tafiti mbalimbali pamoja na ajira

Aidha Dkt Shajak amewasihi wakurugenzi hao kuhakikisha wanazingatia huduma stahiki na nzuri wanazotakiwa kupatiwana Watu wenye Ulemavu na kuona kila penye fursa kunakuwa na mazingatio kwa Watu wenye Ulemavu ili lengo la serikali la kutoa haki na fursa liwe linatekelezwa kwa mujibu wa taratibu

“Nitowe mfano kwa baadhi ya taasisi ambazo zinaajiri mfanyakazi akiwa hana ulemavu na anapopata ulemavu akiwa kazini si busara kumhamishia kwenye taasisi inayosimamia masuala ya Watu wenye Ulemavu bali unachotakiwa kusimamia na kuhakikisha anapata huduma, haki na fursa kulingana na ulemavu wake” alisisitiza Dkt Shajak

Nae Mkurugenzi wa Bi Salma Majid ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mashirikiano makubwa wanayoyapata ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais jambo ambalo limewarahisishia kufikia malengo ya mradi yenye tija na kuelekea Sera ya Serikali ya uchumi wa buluu na kuona Watu wenye Ulemavu wanashirikishwa kwenye masuala ya maendeleo ya kiuchumi katika nchi yao

Mradi wa Mafunzo ya Maendeleo Jumuishi katika Jamii unatekelezwa na zaidi ya nchi 100 duniani ikiwemo Zanzibar na kuendeshwa kwa ushirikiano wa watu wenye ulemavu, familia zao, na jamii taasisi za serikali na zisizo za kiserikali zinazohusiana na utoaji wa huduma za afya, elimu, mafunzo ya amali, huduma za jamii na nyenginezo

Wakitoa ushuhuda kwenye mafunzo hayo juu ya mtazamo wa wanajamii mwalimu wa skuli ya sekondari Mpendae Bi Yumna Mmanga amesema yeye ni mwalimu anaefurahiya kazi yake kwa sababu wanafunzi wake wanajifunza namna nzuri ya kuishi na Watu wenye Ulemavu na kufahamu mahitaji yao, matumizi sahihi ya majina ya Watu wenye Ulemavu na namna ya kuwaita

“naishi nao kirafiki zaidi, napenda wamekuwa wadadisi, na waelewa jambo ambalo linanipa faraja katika kutekeleza majukumu yangu hawanitengi ingawa ninapotembea wakati mwengine wengine hutaka kupiga picha nami wakijua ni mzungu kumbe ni mwanamke mrembo kama wanafunzi wangu wanavyoniita mwalimu mrembo” alisema Yumna

Wakizungumza baada ya mafunzo hayo Mkurugenzi uendeshaji na Utumishi Bakari Khamis kutoka Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora kwa niaba ya Wakurugenzi wameishukuru Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza laTaifa la Watu wenye Ulemavu kwa kuandaa mafunzo hayo jambo ambalo linatoa fursa kwa wakurugenzi kufahamu na kuelewa vyema masuala ya Watu wenye Ulemavu na namna ya ushirikishwaji wao

Nae Mkurugenzi Mipango, sera na utafiti kutoka Wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi Bw Sheha I. Hamdan amesema mafunzo yamekuja kipindi muwafaka cha bajeti ya Serikali kinachopanga mipango ya maendeleo hivyo wanawajibu wa kuhakikisha wanazingatia masuala ya Watu wenye Ulemavu kwa kuweka mazingira wezeshi ili dhana nzima ya uchumi wa buluu kwa wote iweze kufikiwa

Mafunzo hayo yameandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu kwa kushirikiana Mradi wa Mafunzo ya Maendeleo Jumuishi katika Jamii, yalitanguliwa na Makatibu wakuu wa Wizara na Taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo yaliendeshwa na Mwenyekiti wake Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena A. Said yakifuatiwa na Wakurugenzi ambayo yaliongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar D. Shajak

Mada zilizowasilisha ni pamoja na kufahamu dhana ya ulemavu na uzingatiaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu zilizowasilishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu na Dkt Said Khamis kutoka Chuo cha Taifa SUZA ambapo pia washiriki walifahamu aina za ulemavu na sababu zinazopelekea kupata ulemavu

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz