Head image
Govt. Logo

Hits 97976 |  3 online

           


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amewakumbusha wananchi kuwa suala la usafi wa mazingira halihitaji kutengewa siku maalum bali ni wajibu wa kila siku
news phpto

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman amewakumbusha wananchi kuwa suala la usafi wa mazingira halihitaji kutengewa siku maalum bali ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha maeneo wanayokaa mazingira yake yanakuwa safi na salama muda wote

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman amewakumbusha wananchi kuwa suala la usafi wa mazingira halihitaji kutengewa siku maalum bali ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha maeneo wanayokaa mazingira yake yanakuwa safi na salama muda wote

Ameyasema hayo mara baada ya kumaliza kufanya zoezi la usafi wa mazingira katika Hospitali ya Serikali ya Wete akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Mhe Salama Mbarouk ambae ameogozana na viongozi wa mkoa huo akiwemo Mkuu wa Wilaya

Mhe Harusi amewasisitiza wanajamii kujenga utamaduni wa kudumisha usafi wakati wote hasa maeneo ambayo jamii inapata mahitaji ya kibinaadamu kama Hospitali, sokoni, sehemu za kazi kuhakikisha wanadumisha usafi kila baada ya muda ili kulinda afya zao wakati wote

Aidha amewakumbusha wananchi kuzingatia ujumbe wa Siku ya Mazingira Duniani ambao ni “Dunia hii ni moja” ukiwa na maana kutunza na kuhifadhi mazingira ni wajibu wa kila mtu na kinyume chake ni kuiharibu dunia kutokana na maumbile yake

Mhe Harusi pia ameukabidhi uongozi wa Hospitali ya Serikali ya Wete mashuka 300 ya vitanda vya kulalia wagonjwa ambayo yametolewa na Bw Suleiman Moh’d Anadi kwa niaba ya marehemu baba ake Bw Moh’d Anari ambae kabla ya kifo chake alitaka kuyagawa mashuka hao hospitali lakini mauti yalimfikia kabla ya kuwahi kutimiza dhamira yake hio , Mwenyezi Mungu amsamehe amlaze mahala pema Peponi.

Wakati huohuo Mhe Harusi ameshirikiana na wanakikundi chaTulianza Mapema kilioko Tumbe Magharibi kupanda miche ya Mikoko eneo la bondeni ikiwa ni muendelezo wa kutunza na kuhifadhi mazingira hasa katika wiki ya maadhimisho ya sherehe ya siku ya mazingira duniani

Amewahakikishia wanakikundi hao kuwa Serikali inaunga mkono juhudi za wananchi hasa wanaojitolea katika kulinda na kuhifadhi mazingira na kuwaomba wasivunjwe moyo na watu wachache wenye tamaa ambao wanavizia na kuikata mikoko na badala yake wote washirikiane kuwa walinzi wa mazingira ili kumshinda adui wa mazingira

“tunapaswa kuitunza miti na mikoko kwa faida ya vizazi vijavyo na msichoke ili tuendelee kuvuta hewa safi na salama tuzidishe juhudi kulinda na kutunza mazingira na kurudisha uoto wa asili” alitoa msisitizo

Nae Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw Hamad Mwalimu Iddi amemuomba Mhe Harusi kusikia kilio chao na kupatiwa baadhi ya vifaa ikiwemo rainboot, kofia ili wajikinge na jua pamoja na kupatiwa boti kwa ajili ya kufanya doria kwa vile kuna watu wachache ambao huvizia na kuikata mikoko

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Community Forest Pemba (CFP) Bw Mbarouk Mussa Omar amesema jumla ya miche milioni moja na laki mbili imepandwa kwenye eneo la Tumbe bondeni ambapo pia wamekipatia kikundi hicho shilingi milioni tano ili ziweze kusaidia shughuli na mahitaji ya kikundi hicho

Bw Mbarouk ameeleza kuwa Mazingira yanapoharibika viumbe vinaathirika, magonjwa yataongezeka, mvua zitapotea hivyo wajibu wa wanajamii kuchukuwa juhudi za kupanda miti aina mbalimbali ili kurudisha uoto wa asili maana mjenga nchi ni mwananchi

Siku ya mazingira Duniani husherehekewa kilaifikapo tarehe 5 June ambapo kwa Zanzibar mwaka huu kitaifa zinafanyika Pemba mgeni rasmi ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Othman Masoud Othman.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz