Head image
Govt. Logo

Hits 121534 |  16 online

           


Watu wenye ulemavu kisiwani Pemba wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuhesabu watu na makaazi ‘Sensa’ linalotajiwa kuanza Agosti 23
news phpto

Watu wenye ulemavu kisiwani Pemba wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuhesabu watu na makaazi ‘Sensa’ linalotajiwa kuanza Agosti 23 ili nao waweze kujumuishwa katika mipango ya maendeleo.

Watu wenye ulemavu kisiwani Pemba wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuhesabu watu na makaazi ‘Sensa’ linalotajiwa kuanza Agosti 23 ili nao waweze kujumuishwa katika mipango ya maendeleo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa Jumuiya mbali mbali za Watu wenye Ulemavu Pemba kwenye ukumbi wa Idara ya Mazingira Machomanne.

Mhe Harusi amewaomba wazazi na walezi kutokuwaficha watoto wenye ulemavu pamoja na kuficha aina ya ulemavu walionao ili waweze kupatiwa haki yao ya msingi ya kuhesabiwa.

Aidha, amewakumbusha wanajamii na kupigia mstari maneno ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kuhusu kuwapa kipaumbele Watu wenye Ulemavu nchini ili waweze kujumuishwa katika mipango ya maendeleo ya Serikali.

Sambamba na hayo, amewaomba viongozi hao kupambana na vitendo vya udhalilishaji kwa Watu wenye Ulemavu ili kuhakikisha wanaepukana na janga la udhalilishaji ambalo linaonekana kukithiri visiwani Zanzibar.

“niwaombe sana tuwe tayari kupambana na hili janga la udhalilishaji ambalo limeingia katika nchi yetu, wanadhalilishwa watu wenye nguvu zao, wenye macho yao, wenye viungo vyao, wenye akili zao seuze sisi ambao tuna mapungufu fulani, ndugu zangu tulisimamie kwa pamoja” alisisitiza Bi Harusi

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa watu wasioona Pemba Bw Suleiman Mansour, amesema Watu wenye Ulemavu wamelipokea vyema zoezi la Sensa na kuomba makarani wa Sensa kuwa na kauli nzuri kwa Watu wenye Uemavu ili kufanikisha zoezi hilo ipasavyo.

Yahya Mohammed Seif mwenye ulemavu wa uziwi, ameiomba Ofisi ya mtakwimu mkuu wa Serikali kutoa takwimu za Watu wenye Ulemavu ili waweze kutambua Idadi ya Watu wenye Ulemavu nchini na aina ya ulemavu walionao.

Nae, Katibu wa Jumuiya ya Wasioona Wilaya ya Chake Chake Said Abdalla Sadi, ameahidi kuendelea kuwashajihisha Watu wenye Ulemavu kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa pamoja kupambana hali na mali dhidi ya vitendo vya udhalilishaji kwa Watu wenye Ulemavu.

Mratibu wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Kisiwani Pemba Bi Mashavu Juma Mabrouk, amewahimiza washiriki wa Mkutano huo kutoa mashirikiano kwa makarani wa sensa watakapofika kwenye makaazi yao.

Zoezi la Sensa ya watu, makaazi linatarajiwa kuanza tarehe 23 Agost 2022.

Sensa kwa maendeleo, jiandae kuhesabiwa.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz