Mazungumzo ya ushirikiano kuhusu kushughulikia Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira Zanzibar.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar D.Shajak akiwa na Balozi wa Finland Tanzania Bibi Thereza Zitting, kulia ni Naibu Balozi, katikati ni Bi Aziza Juma Ali Afisa Mwandamizi Fedha za Nje OR Fedha na Mipango Zanzibar mara baada ya mazungumzo ya ushirikiano kuhusu kushughulikia Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira Zanzibar. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi ya Uratibu wa SMZ Dar es Salaam.