Head image
Govt. Logo

Hits 116083 |  1 online

           


WATU WENYE ULEMAVU WAPEWA VISAIDIZI
news phpto

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman (alievaa miwani) pamoja na baadhi ya viongozi wa Baraza La Taifa La Watu Wenye Ulemavu wakikabidhi vifaa visaidizi kwa Watu wenye Ulemavu vilivyotolewa na kampuni ya Tanzania Cigarette Public Limite kwenye Ofisi ya Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu iliopo Migombani, Wilaya ya Mjini,Unguja.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais,Zanzibar. Mhe Harusi Said Suleiman ameitaka taasisi ya Tanzania Cigarette Public Limited kuongeza jitihada za utoaji wa msaada kwa jamii hususani kwa Watu wenye Mahitaji Maalumu na Wenye Ulemavu.

Mhe Harus ameyasema hayo wakati akikabidhi vifaa visaidizi vilivyotolewa na kampuni ya Tanzania Cigarette Public Limited vikiwemo Baisikeli 4 za miguu,Magongo ya mkono pisi 40, Magongo ya kwenye Kwapa pisi 40, Fimbo nyeupe pisi 28, mashine za cherehani za kisasa 30 kwa Watu wenye Ulemavu vyenye thamani ya shilingi Milioni 16,322,000.Makabidhiano haya yamefanyika katika ofisi ya Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu, Migombani,Wilaya ya Mjini,Unguja.

Amesema kuna watu wenye mahitaji maalum wanashindwa kupata huduma bora kwa wakati kutokana na hali ngumu inayowakabili.hivyo ipo haja ya kuongeza jitihada za kuwafikia wote wenye kuhitaji mahitaji hayo.

Mhe Harus amefahamisha zaidi kuhusu watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na wale ambao wanaishi katika mazingira magumu kutokana na kufiliwa na wazazi au kuishi na Mzazi moja wa kike.

“Kuna watu maalumu ambao wanaishi na virusi vya ukimwi nao pia wanahitaji msaada maana wanashindwa hata kupata dawa ambazo wanazihitaji, pia kuna mahitaji wanashindwa kuyapata ili waweze kuishi kwani ukizingatia wengine ni mayatima” alisema Mhe Harus.

Aidha,ameeleza kuhusu mpango maalumu wa serikali wa kuirithisha Zanzibar ya kijaani kwa kupanda miti na kurudisha uoto wa asili,ambao unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais,Zanzibar chini ya idara ya Mazingira kwa kushirikiana na Wadau mbali mbali wa mazingira hivyo ameitaka taasisi ya Tanzania Cigarette Public Limited na wadau wengine kuongeza jitihada za kuiunga mkono serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza huu mpango wa kuirithisha Zanzibar ya kijaani.

”Serikali imeandaa programu maalumu’Zanzibar Green Legacy Program’ ya kupanda miti katika maeneo mbali mbali kama vile Kwenye fukwe ili kuirudisha zanzibar ‘green view’ tunawakaribisha rasm ili uendeleza urithi huu” alisema Harus.

Nae,Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu,Mhandisi Ussy Khamis Debe amesema vifaa vilivyotolewa na kampuni ya Tanzania Cigarette Public Limited kwa watu wenye ulemavu vitasaidia na kuwarahisishia kuingia katika ushindani wa soko la kiuchumi na kuchangamkia fursa za ajira zikiwemo kutafuta fursa za uchumi wa buluu.

“Tunafahamu kuwa tunahoteli nyingi zaidi ya holeli 500 zipo Zanzibar hivyo kupitia msaada huu wataingia katika viwanda vya ushoni na watapata kujikamua kiuchumi”

Vilevile,Mkurugenzi wa kampuni ya Tanzania Cigarette Public Limited, Ndg,Oscar Lwoga amesema katika kuboresha maisha ya watanzania wanaendelea kuiunga mkono serikali kwa kuwapatia vitendea kazi Watu wenye ulemavu ambao wapo wanasoma elimu za juu vyuoni kwa kuwapatia vifaa saidizi vitakavyowasaidia katika masomo yao na vilevile kuwasaidia wajasiria mali ndani ya jamii ili kupunguza changamoto zao na pia kushiriki katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

“Katika shughuli za kusaidia jamii huwa tuna mambo matatu,kwanza, tunawasaidia watu wenye ulemavu ambao wapo kwenye jamii na ambao wapo vyuo vya elimu ya juu haswa wale wanahitaji vifaa vya kusomea pia kuwasaidia vikundi vya wajasiria mali kulingana na mahitaji yao ya kila siku na kwa upange wa mazingira huwa tunapanda miti,tunafanya usafi wa miji,tunatoa vifaa vya usafi au kutoa miche ya kupanda”amesema Oscar.

Akitoa shukurani kwa niaba ya wenzake mmoja wa waliopata msaada huo Khatib Nassor Khatib alisema msaada walioupata utasaidia kuondokana na changamoto zinazowakabili na kuiomba serikali iendelee kuwajali kwa kuwapatia vifaa tofauti tofauti kulingana na mahitaji yao.

“Kwa niaba yangu na wenzangu tumefurahi sana na tunatoa shukurani za dhati kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu kwa juhudi wanazozichukua katika kutusaidia,lakini pia tunaishukuru Kampuni ya Tanzania Cigarette Public Limited kwa kutujali na kuona umuhimu wa kuja kutusaidia hivyo iendelee kusiwe ndio mwisho,”alisema Khatib.

Hafla ya kukabidhi vifaa visaidizi imefanyika huko katika Ofisi ya Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu,Migombani,wilaya ya Mjini,Unguja. ambapo kampuni ya Tanzania Cigarette Public Limited ikitoa vifaa visaidizi vyenye thamani ya shilingi Milioni 16,322,000 kwa Watu wenye ulemavu ambavyo ni Baiskeli 4 za miguu,Magongo ya mkono pisi 40, Magongo ya kwenye Kwapa pisi 40, Fimbo nyeupe pisi 28, mashine za cherehani za kisasa 30.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz