Head image
Govt. Logo

Hits 121604 |  7 online

           


USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI (COP 28)

COP 28 ni mkutano wa 28 wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa(UN) wa hali ya hewa.Kulingana na Mabadiliko ya tabianchi duniani na mahitaji makubwa ya kudhibiti athari za Mabadiliko ya tabianchi ,Serikali ya Umoja wa mataifa huandaa mikutano maalumu kila mwaka kujadili mabadiliko na jinsi ya kuweka kikomo ili kujiandaa kwa mabadiliko yajayo ya tabia nchi.

COP inasimama kwa “Mkutano wa Vyama”Pande hizo ni nchi zilizotia saini makubaliano ya awali ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa mwaka 1992.

Viongozi wa dunia wanatazamiwa kujadili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa mjini Dubai ambapo mtendaji mkuu wa kampuni ya mafuta inayomilikiwa na Serikali,Sultan Al Jaber kuwa Rais wa mazungunzo ya COP28.

Tanzania ni mingoni mwa nchi zitakazoshiriki katika mkutano wa COP 28 ambapo jumla ya washiriki takriban 100 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanatarajiwa kushiriki.Zaidi ya nchi 800 zimealikwa kutoka mataifa mbali mbali duniani .kulingana na agenda Tanzania itaangazia Biashara ya Kaponi,Uchumi wa Bluu,Kilimo Endelevu na Nishati Safi ya Kupikia ambapo kaulimbiu ya taifa ni “kuimarisha kilimo Himilivu na Uchumi wa Bluu katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi”.

Mkutano huu pia unalenga kuongeza chachu ya uwekezaji wa kimataifa kwa kutumia fursa katika sekta kwa kuvutia wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali duniani kote ili kufahamu fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania.

Matarajio ya COP 28 ni pamoja na kuhakikisha msimamo wa Tanzania unakubaliwa, kupata fursa za upatikanaji wa rasilimali fedha kuwezesha utekelezaji wa miradi pamoja na teknolojia za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Pia, nchi inatarajia kuongeza uwekezaji katika Biashara ya Kaboni, kutangaza jitihada za nchi na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kulingana na matarajio ya UN COP28 itasaidia kuweka hai lengo la kupunguza ongezeko la joto duniani kwa muda mrefu hadi 1.5C. Hii ilikubaliwa na karibu nchi 200 huko Paris mnamo 2015.

Lengo la 1.5C ni muhimu ili kuepuka athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi kulingana na shirika la hali ya hewa la Umoja wa Mataifa, Jopo la Kiserikali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC).

“Ongezeko la joto la muda mrefu kwa sasa linasimama karibu 1.1C au 1.2C ikilinganishwa na nyakati za kabla ya viwanda, kipindi kabla ya wanadamu kuanza kuchoma nishati ya mafuta kwa kiwango kikubwa”UN inasema.

Mkutano huo utafanyika Dubai,katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE),kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz