Tume ya UKIMWI ZANZIBAR ikiongozwa na OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS imeadhimisha Siku ya UKIMWI DUNIANI katika Viwanja vya Skuli ya Nungwi, tarehe 01 Disemba. huu ni muendelezo wa kuratibu Maadhimisho haya kwa kila Mwaka ifikapo Disemba Mosi
Madhumuni ya maadhimisho haya ni kutathmini hali na mwelekeo wa UKIMWI Kitaifa na Kimataifa.
Aidha Siku hii hutumika kuhamasisha na kuelimisha jamii juu ya namna bora ya kujikinga na Maambukizi Mapya ya VVU,Matumizi sahihi ya ARV kwa watu wanaoishi na VVU pamoja na Kupinga ubaguzi na Unyanyasaji wanaofanyiwa watu wanaoishi na VVU.
Maadhimisho ya Kitaifa kwa upange wa Zanzibar yamefanyika katika kijiji cha Nungwi ambapo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa OTHMAN MASOUD OTHMAN alikuwa Mgeni Rasmi.
Kwa Mujibu wa Tume ya UKIMWI ZANZIBAR,Kaulimbiu ya Maadhimisho haya ya mwaka huu ni “JAMII ZIWEZESHWE KUONGOZA MAPAMBANO YA UKIMWI”
Kauli mbiu hii inasisitiza uwezeshaji katika shughuli za kudhibiti UKIMWI kuanzia kwenye rasilimali fedha za utoaji wa huduma za VVU pamoja na upangaji wa mikakati ya Kupambana na UKIMWI.