Head image
Govt. Logo

Hits 98053 |  4 online

           


MAADHIMISHO YA SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI

Baraza la Taifa La Watu wenye Ulemavu linatarajia kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani katika Ukumbi wa POLISI ZIWANI Wilaya ya Mjini Unguja,kesho tarehe 03 Disemba 2023.huu ni uratibu na muendelezo wa kila mwaka kuadhimisha Siku hii.

Katika Kilele cha Maadhimisho haya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar MHE. OTHMAN MASOUD OTHMAN atakuwa Mgeni rasmi.

Maadhumuni ya maadhimisho haya yana lengo la kuhamasisha jamii kuweza kupata uelewa wa masuala ya watu wenye ulemavu na kujitathmini juu ya upatikanaji wa haki na fursa ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Pia inalenga kuongeza ufahamu wa mafanikio yatakayopatikana kutokana na ushirikiano wa Watu wenye Ulemavu katika kila nyanja za maisha ya kisiasa,kijamii,kiuchumi na kiutamaduni.Na kuhakikisha kuwa lengo la kukuza uelewa wa masuala ya Ulemavu na uungwaji mkono kwa ajili ya utu,heshima,haki,ustawi,mafao na maendeleo ya watu wenye Ulemavu linafikiwa.

Kwa Mujibu wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inasema ‘’TUUNGANE PAMOJA KATIKA KUCHUKUA HATUA ILI KUFIKIA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU KWA WATU WENYE ULEMAVU”

Kauli mbiu hii imezingatia mambo muhimu ikijumuisha malengo ya maendeleo endelevu kwa Watu wenye Ulemavu kama vile; lengo la kuondosha umasikini uliokithiri,uwepo na usawa wa kijinsia kwa wote bila ya kujali utofauti wa mtu kwa upange wa elimu.uwepo wa afya bora na ustawi mzuri kutokana na hali duni walizonazo na uwepo wa miundombinu rafiki na wezeshi kwa watu wenye ulemavu katika sehemu za upatikanaji wa huduma.

Kiujumla Siku hii imepewa kipaumbele, umuhimu na ulazima wa kuadhimishwa kila mwaka duniani kote kwa nchi wanachama zilizoridhia Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu wa mwaka 2006 ambapo Tanzania umeridhiwa mwaka 2009.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz