Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Harusi Said Suleiman akiwa katika ziara ya kushtukiza yenye lengo la kukagua Mazingira na kutoa Elimu ya Utunzaji Salama wa Takataka zilizopo pembezoni mwa Bahari katika Hoteli ya TUI BLUE,Mkoa wa Kaskazini,Unguja:tarehe 21 Februari,2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Harusi Said Suleiman amewataka viongozi wa Hoteli ya TUI BLUE ZANZIBAR kuongeza juhudi za utunzaji salama wa Mazingira pamoja na Takataka hatarishi zilizopo pembezoni mwa bahari ili kuongeza haiba ya Zanzibar pamoja na Utalii kiujumla.
Ameyasema hayo mara baada ya kukagua Takataka,katika ziara ya kushtukiza yenye lengo la kukagua Mazingira na kutoa Elimu ya Utunzaji Salama wa Takataka zilizopo pembezoni mwa Bahari.
Katika Ziara hiyo,Mhe,Harusi amefanya pia zoezi la Ukusanyaji wa Mwani unaochanyanyika katika Takataka hizo.