Head image
Govt. Logo

Hits 116813 |  1 online

           


ZANZIBAR HAIZALISHI DAWA ZA KULEVYA ZINAINGIZWA__WAZIRI HARUSI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Harusi Said Suleiman amesema kulingana na utafiti imebainika kuwa Dawa za Kulevya zinapitishwa nchini kupitia njia mbali mbali kuelekea sehemu nyengine zilizopo karibu na Zanzibar ila kabla ya kuwasili katika sehemu iliyokusudiwa zinaanza kufanya kazi hapa nchini.

Ameyasema hayo Februari 29,2024 kwenye Baraza la 10 la Wawakilishi-Mkutano wa 14-kikao cha 12 wakati alipokuwa akifanya Majumuisho ya taarifa ya Dawa za kulevya nchini.

“Dawa za Kulevya hazikukusudiwa zitumike hapa,lakini kwasababu ya Wateja wapo zinaanza kutumika hapa na baadae zinapelekwa sehemu walipokusudia” alisema Waziri Harusi.

Mhe.Harusi amefafanua njia maarufu zinazotumika kusafirishia Dawa za kulevya dunian na kuingia hapa nchini ambazo ;ni njia ya Afghanstan kupitia Pakistani na Myanmar kuelekea nchi ya Ulaya na Marekani hutumika kusafirishia Heroine,njia ya Latin Amerika na maeneo ya kusini mwa Afrika hutumika kusafirishia kokain, na Bangi huingia nchini kupitia Afghanstan na baadhi ya maeneo ya Tanzania Bara,Afrika ya Kusini na Mombasa Kenya.

Halikadhalika,Mhe.Harusi amewashukuru wananchi na kuwataka kutoa taarifa kamili za wauzaji na waingizaji wakubwa wa Dawa za Kulevya ili kunusuru kizazi cha sasa na baadae.

“Tusikubali kutengeneza generation nyengine ya Dawa za Kulevya,tutibu hii tuliyokuwa nayo” Alisisitiza Waziri Harusi.

Pia Mhe.Harusi amewataka wazazi na walezi kuwafatilia watoto wao ambao wapo mashuleni ili kuweza kuwanusuru na janga hili la matumizi ya Dawa za Kulevya.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz