Head image
Govt. Logo

Hits 120667 |  3 online

           


WAZIRI HARUSI AUNGANA NA KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZIARA YA EBARR MOROGORO.
news phpto

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Harusi Said Suleiman akiwa na Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi inayoongozwa na mwenyekiti wake Mhe.Machano Othman Said pamoja na kamati ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais katika ziara ya kukagua Mradi wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mfumo Ikolojia Vijijini (EBARR) katika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro:tarehe 09 Machi ,2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Harusi Said Suleiman ameongozana na Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi inayoongozwa na mwenyekiti wake Mhe.Machano Othman Said pamoja na kamati ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais katika ziara ya kukagua Mradi wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mfumo Ikolojia Vijijini (EBARR) katika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro:tarehe 09 Machi ,2024.

Amekagua miradi ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata bidhaa za ngozi wenye thamani ya Tsh 108,010,000, uchimbaji wa lambo kwa ajili ya kueneza technolojia ya uvunaji wa maji wenye thamani ya Tsh 293,654,565.32 na mradi wa shamba la uzalishaji wa uyoga wenye thaman ya Tsh 5,500,00 katika kijiji cha Melea.

Vilevile katika kijiji cha Mingo na Lubungo amekagua mradi wa kisima kirefu cha umwagiliaji wa mazao ya mbogamboga kwa kutumia umeme jua (Solar) wenye thamani ya Tsh milioni 74.8 na mradi wa uzalishaji wa Samaki katika mabwawa wenye thamani ya Tsh milioni 22.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo,Mhe.Harusi ameishukuru na kuipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuratibu vyema mradi huo unaotekelezwa katika pande zote mbili za Muungano.

Amesema mradi huo umeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa wilaya ya Mvomero kwa kuweza kupata ajira ambayo inawasaidia katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

Aidha,Mhe.Harusi amewataka wasimamizi wa mradi huo kuendelea kuutunza na kuudumisha ili uendelee kuleta tija zaidi kwa wananchi na kuwarahisishia kupata huduma za kijamii zikiwemo maji yanayowasaidia katika shughuli za kilimo na ufugaji.

“Mmepata mradi wa kujiendeleza,malengo ya serikali zote mbili(Muungano) kuwafanya wananchi wake kujiajiri na kuweza kupata kipato cha kujiendesha katika maisha,huu mradi utawafanya mujiajiri nyinyi na watu walokuwa karibu na kijiji,kwa niaba ya Kamati nawaomba muudumishe” amesema waziri Harusi.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa kamati ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa ya Baraza la wawakilishi.Mhe.Mchano Othman Said amesema mradi huo utawasaidia wananchi katika kujikamua na umasikini na kuwarahisishia kupata huduma za kijamii kwa urahisi, hivyo Mhe Machano amewahimiza wananchi kuitumia miradi hiyo kujipatia huduma za kijamii hususan maji kutokana na visima na malambo yanayojengwa katika maeneo yao kupitia miradi hiyo ya mazingira.

Pia,Mhe.Machano amewataka wananchi kuendelea kuthamini mchango wa Serikali zote mbili (Muungano) katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

“Serikali ya Mama na Serikali ya awamu ya sita ndio inasimamia mradi huo,mradi ambao lengo lake ni kuwakomboa wananchi wilaya ya Mvomero katika umasikini” amesema Mhe.Machano.

Mradi wa EBARR unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) unatekelezwa katika wilaya za Mvomero (Morogoro), Mpwapwa (Dodoma), Simanjiro (Manyara), na Kishapu (Shinyanga) kwa upande wa Bara na Matemwe (Unguja) kwa upande wa Zanzibar.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz