Head image
Govt. Logo

Hits 118749 |  1 online

           


MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI TAREHE 05 JUNI, 2024

Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar kupitia sekta ya Mazingira (ZEMA na DOE) inatarajia kuadhimisha Siku ya Mazingira duniani katika Wilaya ya Micheweni -Pemba, tarehe 05 Juni,2024 .Huu ni utaratibu na muendelezo wa kila mwaka kuadhimisha siku hii.

Katika Kilele cha Maadhimisho haya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar MHE. OTHMAN MASOUD OTHMAN atakuwa Mgeni rasmi.

Madhumuni ya maadhimisho haya ni kuhamasisha jamii duniani kote kuelewa masuala ya mazingira na pia kuhamasisha watu wa jamii mbalimbali duniani kuwa mstari wa mbele katika kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inasema:

“TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUPANDA MITI KUIENDELEZA ZANZIBAR YA KIJANI”

Msingi wa kaulimbiu ya Zanzibar ni kuwahamasisha na kuwawezesha wananchi wote wa Zanzibar na wadau kuelewa umuhimu wa misitu, kuhifadhi miti iliyopo, kupanda na kuikuza miti ili kuimarisha mazingira kwa ajili ya Kizazi cha sasa na cha baadae.

Utekelezaji wa kaulimbiu hii kutainufaisha jamii ya Zanzibar kwa jumla kwa kupunguza uwezekano wa kuathiriwa na

mabadiliko ya tabianchi na hasara nyengine za kimazingira, na kusaidia Zanzibar kufikia kuwa na mazingira endelevu kwa faida ya kiuchumi na kijamii.

Kiujumla Siku hii imepewa kipaumbele,umuhimu na ulazima wa kuadhimishwa

kila mwaka duniani kote kwa nchi zilizoridhia Mkataba wa

Kimataifa wa Mazingira, na Baraza la Umoja wa Mataifa mwaka 1972, wakati wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira uliofanyika Stockholm, Nchini Sweden.

Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mazingira Dunia yatafanyika Riyadh- Saudi Arabia chini ya kaulimbiu ya

“ land restoration,desertification and drought resilience” kauli hii ina maana kuwa tuendeleze ardhi yenye uharibifu wa Mazingira, kuokoa majangwa na kuifanya ardhi kuwa stahamilivu na mabadiliko ya Tabianchi.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz