Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Bi. Maryam Juma Abdallah (kati) akipokea barua ya makabidhiano ya gari aina ya Toyota Hilux Double Cabin kwa matumizi ya Mradi wa Kuimarisha Uhimili wa Mabadiliko ya Tabianchi kwa Jamii za pwani ya Zanzibar unaofadhiliwa na Mfuko wa Fedha za Mazingira ( ADAPTATION FUND )chini ya Usimamizi wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutoka kwa Mwakilishi wa NEMC ndugu. Nice Mshana.
Pembeni kulia ni walioshuhudia ni Mkurugenzi Idara ya Mazingira ndugu. Farhat Ali Mbarouk, Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi ndugu. Juna Ali Simai wakiwa pamoja na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
Akizungunza mara baada ya makabidhiano hayo, Katibu Mkuu Maryam amesema ujio wa gari hio utasaidia na kuwezesha kutekelezaji wa kazi za mradi kwa wepesi na ufanisi pamoja na kupunguza changamoto ya usafiri iliyokuwepo awali.
Hatahivyo, amesema Ofisi yake inaendelea vyema na kutekeleza mikakati ya Usimamizi wa Mazingira ili kuhakikisha inakabiliana vyema na mabadiliko ya tabianchi yanayoikubwa Zanzibar na Dunia kiujumla.
Aidha, zoezi hili la makabidhiano ya gari limefanyika katika makao makuu ya Ofisi hii iliyopo Migombani - Unguja: tarehe 04 Juni. 2025.
Nemc Tanzania