Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar

📢

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Kwanza wa Rais

Madhumuni

Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Kwanza wa Rais inafanya kazi za kuratibu shughuli zote za Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais na kutoa huduma zote muhimu kwa Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais na familia yake pamoja na kutunza makaazi ya Makamu wa Kwanza wa Rais yaliyoko Mazizini Unguja. Majukumu mengine ya Ofisi ya Faragha ni kama yafuatayo:-

Kazi za Ofisi

  • Kuwa ni msingi wa mawasiliano baina ya Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Serikali hasa viongozi na wananchi.
  • Kumsaidia Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika masuala yote ya kuimarisha mahusiano na jamii
  • Kutunza makaazi ya Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais yaliyoko Mazizini Unguja.
  • Kufanya tafiti kutambua na kuchunguza maeneo yenye udhaifu katika ufikishwaji wa huduma za haki, kutayarisha na kutekeleza mbinu za kupunguza/kuondosha malalamiko hayo
  • Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ahadi za Mheshimiwa Makamu wa Rais alizozitoa kwa wananchi.
  • Kuimarisha mashirikiano na mahusiano ya Kitaifa na Kimataifa kwa kukutana na Mabalozi na Wageni Mashuhur; na
  • Kuratibu ziara za Mheshimiwa Makamu wa Kwanza za ndani na nje ya nchi

IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI

Madhumuni

Kutoa huduma za kitaalam za utawala, uendeshaji na usimamizi wa rasilimali watu ya Wizara.

Kazi za Idara

  • Kutoa ushauri wa kimkakati wa uendeshaji na usimamizi wa rasilimali watu yakiwemo ajira, maendeleo ya rasilimali watu, mafunzo, nidhamu, ubakizaji watumishi, usimamizi wa utendaji, na maslahi wa watumishi..
  • Kuhakikisha matumizi sahihi, na usimamizi wenye ufanisi wa rasilimali watu kwenye Wizara.
  • Kukusanya, Kuchambua, kuhifadhi, taarifa za rasilimali watu, na kusambaza taarifa za mipango ya maendeleo ya rasilimaki watu.
  • Kutoa ushauri kwa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu maudhui na matumizi ya Sera ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Sheria za Utumishi wa Umma
  • Kutoa takwimu na taarifa mbali mbali za rasilimali watu za wakati uliopo
  • Kutoa hududma za kiutawala na maendeleo ya kitaasisi.
  • Kuandaa na kushughulikia mafao ya watumishi wanaoacha kazi.
  • Kutoa ushauri kwa Katibu Mkuu kuhusu mambo ya rasilimali watu
  • Kutafsiri na kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbali mbali zinazoagizwa na mamlaka mbalimbali

Idara hii imegawika katika sehemu kuu mbili, nazo ni

Majukumu

  • Kutafsiri na kuhakikisha uzingatiaji wa Kanuni za Utumishi wa Umma, Kanuni za Kudumu na sheria za Kazi.
  • Kuwezesha uwepo wa mahusiano stahili miongoni mwa watumishi.
  • Kusimamia masuala yote ya itifaki.
  • Kusimamia huduma za ulinzi, usafirishaji na usafi wa mazingira.
  • Kusimamia huduma za vifaa vya ofisi, matengenezo ya majengo, na usafi wa ofisi.
  • Kuratibu uzingatiaji wa maadili na thamani ya heshima Wizarani.
  • Kusimamia uzingatiaji wa masuala mtambuka kama jinsia, watu wenye ulemavu, VVU/UKIMWI na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
  • Kuratibu utekelezaji wa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika wizara.
  • Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa bajeti ya mwaka ya Idara ya Utawala.
  • Kuratibu utekelezaji wa Mkakati wa kuinua kiwango cha utendaji ndani ya wizara na Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Client Service Charter).

Majukumu

  • Kuratibu ajira na uteuzi wa watumishi wapya, upangaji, kuthibitishwa kazini, upandishwaji vyeo, na uhamisho ndani ya wizara.
  • Kutoa huduma za masjala, utarishi, na kumbukumbu za ofisi.
  • Kuandaa mpango wa rasilimali watu na kutambua mahitaji ya wataalamu wa wizara.
  • Kusimamia maandalizi na malipo ya mishahara.
  • Kuratibu utekelezaji wa mfumo wa wazi wa upimaji utendaji kazi, kutathmini matokeo, kuandaa taarifa, na kufuatilia utekelezaji.
  • Kushughulikia likizo mbalimbali za watumishi.
  • Kuandaa mafao na stahili za watumishi wanaoondoka kazini.
  • Kuandaa makisio ya mishahara na posho za watumishi za mwaka.
  • Kuandaa na kuwezesha utekelezaji wa mpango wa mfululizo wa kurithishana ndani ya wizara.
  • Kuwezesha mafunzo kazini kwa watumishi wapya wa wizara.
  • Kuendesha tathmini ya mahitaji ya mafunzo, kupanga mafunzo, na kufuatilia utekelezaji ndani ya wizara.
  • Kutekeleza jukumu la huduma za Sekreterieti ya Kamati ya Ajira na Maendeleo ya Watumishi ya wizara.
  • Kupokea, kuchambua na kuratibu taarifa mbalimbali zinazohusu rasilimali watu ndani ya wizara na taasisi zake.

IDARA YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI

Madhumuni

Kutoa huduma za utaalamu za ushauri katika utungaji na uandaaji wa sera, mipango, na kuongoza kazi ya tathmini na ufuatiliaji kwenye Wizara.

Kazi za Idara

  • Kuratibu maandalizi ya sera za kisekta, kufuatilia utekelezaji na kufanya tathmini ya athari zake.
  • Kuchambua sera za sekta nyingine na kutoa ushauri ipasavyo.
  • Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mipango na bajeti ya wizara, na kufanya tathmini na ufuatiliaji wa mipango na bajeti hizo.
  • Kutekeleza mipango ya udhibiti wa athari (risk management plan).
  • Kufanya tafiti, tathmini na ufuatiliaji wa mipango ya wizara.
  • Kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa huduma za sekta binafsi wizarani.
  • Kuratibu michango ya wizara kwa hotuba ya bajeti na ripoti ya uchumi ya mwaka.
  • Kurasimisha uandaaji wa mipango ya kimkakati, bajeti, tathmini na ufuatiliaji wizarani.
  • Kufanya tafiti na chambuzi za kina kwenye sekta ya sheria na kutambua maeneo yanayohitaji kuwekewa sera.
  • Kuandaa mipango ya sekta ya sheria ya muda mfupi na mrefu.

Idara hii imegawika katika sehemu kuu mbili, nazo ni

Majukumu

  • Kuandaa, kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa sera za Wizara.
  • Kuchambua na kutoa ushauri kwa sera zinazotungwa na wizara nyingine.
  • Kufanya utafiti wa athari za sera mbalimbali na kutoa ushauri wa namna ya kuzifanyia kazi.
  • Kuratibu uandaaji na kufanya mapitio ya sera za Kiwizara.
  • Kushiriki uchambuzi wa shughuli (zisizo za msingi wizarani) zinazoweza kufanywa na asasi za nje (outsourcing) na ushirikishwaji wa sekta binafsi, na kuliwekea sera stahili.
  • Kutafsiri na kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa sera mbalimbali zinazoagizwa na mamlaka mbalimbali.
  • Kupokea, kuchambua na kuratibu maoni ya wadau na kuandaa mapendekezo ya uundaji au marekebisho ya sera mbalimbali kutoka sekta au taasisi husika.
  • Kufanya tafiti na kutoa mapendekezo ya sera kwa masuala ya sekta na sheria.

Majukumu

  • Kuratibu uandaaji wa Mpango Mkakati wa muda wa Kati, na mipango ya utekelezaji ya mwaka na bajeti.
  • Kuratibu na kuandaa Hotuba ya Bajeti ya Wizara.
  • Kukusanya taarifa za utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi na za Kamati za Bunge.
  • Kukusanya taarifa za miradi ya Wizara, programu na kutengeneza mikakati ya upatikanaji wa rasilimali.
  • Kushirikisha Wizara ya Fedha na OR Utumishi wa Umma kwenye mchakato wa utengenezaji wa Mpango Mkakati na Bajeti.
  • Kutoa maelekezo ya kitaalam katika kurasimisha uundaji wa Mpango Mkakati na bajeti kwa idara za ndani ya Wizara.
  • Kushiriki uchambuzi wa shughuli (zisizo za msingi wizarani) zinazostahili kufanywa na asasi za nje ya serikali (outsourcing) na ushirikishwaji wa sekta binafsi.

Kitengo cha TEHAMA

Kazi za kitengo hiki ni pamoja na...

Scroll to Top