MUHTASARI WA MAELEZO YA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS
Utangulizi
Kimuundo Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, inaongozwa na Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye anasaidiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Mtendaji Mkuu wa Ofisi ni Katibu Mkuu ambaye anasaidiwa katika utekelezaji wa majukumu ya Ofisi kupitia wakuu wa Taasisi na Idara.
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inaundwa na Taasisi tatu zinazojitegemea na Idara sita ambazo ziko chini ya Ofisi ya Katibu Mkuu. Kwa upande wa Taasisi zinazojitegemea ni Tume ya UKIMWI, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (ZEMA) na Idara zilizopo chini ya Ofisi ya Katibu Mkuu ni Ofisi ya Faragha, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Idara ya Uendeshaji na Utumishi, Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu, Idara ya Mazingira na Ofisi Kuu Pemba.
Ofisi ya Faragha ndio yenye dhamana ya kusimamia na kuhakikisha kwamba kazi na shughuli za Makamu wa Kwanza wa Rais zinafanyika kwa ufanisi mkubwa.
Dira
Kuwa na usimamizi madhubuti na endelevu wa mazingira, jamii iliyoepukana na matumizi ya dawa za kulevya na maambukizi ya VVU/UKIMWI pamoja na uhifadhi wa haki za Watu Wenye Ulemavu.
Dhamira
Kuratibu jitahada za kisekta kwa usimamizi mzuri wa mazingira, udhibiti wa dawa za kulevya na maambukizi ya VVU/UKIMWI pamoja na kulinda haki na fursa za Watu wenye Ulemavu.
Majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
-
Kuratibu na kusimamia mambo yote yanayohusu Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Kwanza wa Rais;
-
Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Mipango, Sera na Sheria za Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais;
-
Kuratibu masuala ya Watu wenye Ulemavu;
-
Kuratibu na kusimamia masuala ya Mazingira;
-
Kuratibu na kusimamia masuala ya VVU/UKIMWI; na
-
Kuratibu na Kusimamia Udhibiti na Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya.
OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS INAUNDWA NA TAASISI ZIFUATAZO
-
OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS
-
IDARA YA FARAGHA YA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS
-
IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI
-
BARAZA LA TAIFA LA WATU WENYE ULEMA
-
IDARA YA MAZINGIRA
-
MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA MAZINGIRA
-
MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUZUIA DAWA ZA KULEVYA
-
TUME YA UDHIBITI WA UKIMWI
-
-
IDARA YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI
-