Kikao hiki kinalenga kufanya mapitio ya pamoja kati ya Baraza na Mtaalamu Elekezi kuhusu hatua ya maendeleo ya mifumo na tovuti ambayo bado haijakamilika kwa asilimia 100. Lengo ni kujua tumefikia wapi, changamoto zilizopo, na kuweka makubaliano ya muda wa kukamilisha kazi.