Head image
Govt. Logo

Hits 110366 |  3 online

           


IDARA YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI

Madhumuni

Kutoa huduma za utaalamu za ushauri katika utungaji na uandaaji wa sera, mipango, na kuongoza kazi ya tathmini na ufuatiliaji kwenye Wizara.

Kazi za Idara

  1. Kuratibu maandalizi ya sera za kisekta, kufuatilia utekelezaji na kufanya tathmini ya athari zake.
  2. Kuchambua sera za sekta nyingine na kutoa ushauri ipasavyo
  3. Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mipango na Bajeti ya Wizara na kufanya tathmini na ufuatiliaji wa mipango na Bajeti hizo
  4. Kutekeleza Mipango ya udhibiti wa athari (risk management plan)
  5. Kufanya tafiti, tathmini na ufuatiliaji wa mipango ya Wizara.
  6. Kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa hududma za sekta binafsi Wizarani
  7. Kuratibu michango ya Wizara kwa Hotuba ya Bajeti na Ripoti ya Uchumi ya Mwaka.
  8. Kurasimisha uandaaji wa mipango ya kimkakati, bajeti, tathmini na ufuatiliaji wizarani.
  9. Kufanya tatfiti na chambuzi za kina kwenye sekta ya sheria na kutambua maeneo yanayohitaji kuwekewa sera
  10. Kuandaa mipango ya sekta ya sheria ya muda mfupi na mrefu

Idara hii imegawika katika sehemu kuu mbili, nazo ni

  • Sehemu ya Uratibu wa Sera na Tafiti

    Majukumu

    1. Kuandaa, kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa sera za Wizara
    2. Kuchambua na kutoa ushauri kwa sera zinazotungwa na wizara nyingine.
    3. Kufanya utafiti wa athari za sera mbalimbali na kutoa ushauri wa namna ya kuzifanyia kazi
    4. Kuratibu uandaaji na kufanya mapitio ya sera za Kiwizara
    5. Kushiriki uchambuzi wa shughuli (zisizo za msingi wizarani) ambazo zinaweza kufanywa na asasi za nje (outsourcing) na ushirikishwaji wa sekta binafsi na kuliwekea sera stahili
    6. Kutafsiri na kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa sera mbali mbali zinazoagizwa na mamlaka mbalimbali
    7. Kupokea kuchambua na kuratibu maoni ya wadau na kuandaa mapendekezo ya uundaji ama marekebisho ya sera mbalimbali kutoka sekta ama taasisi husika.
    8. Kufanya tafiti na kutoa mapendekezo ya sera kwa masuala ya sekta na sheria.
  • Sehemu ya Mipango, Tathmini na Ufuatiliaji

    Majukumu

    1. Kuratibu uandaaaji wa Mpango Mkakati wa muda wa Kati, na Mipango ya utekelezaji ya mwaka na Bajeti
    2. Kuratibu na kuandaa Hotuba ya Bajeti ya Wizara
    3. Kukusanya taarifa za utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi na za Kamati za Bunge
    4. Kukusanya Taarifa za Miradi ya Wizara, Programu na kutengeneza mikakati ya upatikanaji wa rasilimali.
    5. Kushirikisha Wizara ya Fedha na OR Utumishi wa Umma kwenye mchakato wa utengenezaji Mpango Mkakati na Bajeti
    6. Kukusanya Taarifa za Miradi ya Wizara na Programu, na kutengeneza mikakati ya upatikanaji wa rasilimali.
    7. Kutoa maelekezo ya kitaalam katika kurasimisha uundaji wa Mpango Mkakati na bajeti kwa Idara za ndani ya Wizara.
    8. Kushiriki uchambuzi wa shughuli(zisizo za msingi wizarani) zinazo stahili kufanywa na asasi za nje ya serikali (outsourcing) na ushirikishwaji wa sekta binafsi

IDARA YA MAZINGIRA

Idara ya Mazingira ni miongoni mwa taasisi ziliomo ndani ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ambayo jukumu lake kubwa ni kuhakikisha kuwa nyezo za usimamizi wa mazingira (environmental management tools) ikiwa ni pamoja na sera, sheria, kanuni, mikakati na miongozo inakuwepo; kutoa elimu ya Mazingira kwa jamii pamoja na kuratibu masuala ya mabadiliko ya tabianchi Zanzibar. Nyenzo kuu za kuhakikisha kuwa malengo ya kuundwa kwa Idara yanafikiwa ni pamoja na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar mwaka 2050, Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 Sera ya Mazingira ya mwaka 2013; Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2015 na Kanuni zake; Sera na Sheria za kisekta zinazohusiana na maliasili.

DHAMIRA (Mission)
Kuimarisha nyezo stahiki za usimamizi wa mazingira; pamoja na kujenga uwezo na kutekeleza hatua za kujihami na kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi (Promote required environmental management tools; and capacity development and implementation of actions towards adaptation and mitigation against climate change).

DIRA (Vision)
Kuwa na Zanzibar yenye mazingira endelevu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho (Zanzibar with sustainable environment for future and present generation).

MAJUKUMU YA IDARA YA MAZINGIRA

  1. Kutayarisha mikakati na miongozo ya kitaifa ya usimamizi wa mazingira;
  2. Kuratibu utekelezaji wa mikakati ya kitaifa na miongozo ya usimamizi wa mazingira;
  3. Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa Mkakati wa Tathmini ya Kimazingira kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2015.
  4. Kupendekeza viwango vya kimazingira.
  5. Kuratibu utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya kimazingira.
  6. Kuandaa na kutoa ripoti ya hali halisi ya kimazingira kwa Zanzibar na kuwasilishwa kwa Waziri katika kila kipindi cha miaka mitano.
  7. Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Mazingira.
  8. Kuratibu masuala ya mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na shughuli za kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko hayo.
  9. Kuendeleza elimu ya mazingira kwa jamii na wadau wengine kwa mujibu wa majukumu yake.
  10. Kuratibu na kuendeleza utafiti wa kimazingira na
  11. Kutekeleza kazi nyengine yoyote katika kufanikisha utekelezaji wa Sheria hii.

MUUNDO WA IDARA YA MAZINGIRA

Idara inazo Sehemu Kuu (section) sita (6) ambazo zinaongozwa na Wakuu wa Sehemu. Sehemu hizo ni:

  1. Mabadiliko ya Tabianchi
  2. Mipango, Sera na Utafiti
  3. Elimu ya Mazingira
  4. Utawala na Fedha
  5. Hifadhi ya Bioanuwai
  6. Ofisi ya Idara - Pemba

MAJUKUMU SEHEMU NA IDARA

Sehemu ya Mabadiliko ya Tabianchi.

  1. Kuratibu shughuli mbali mbali za usimamizi wa mabadiliko ya tabianchi.
  2. Kuratibu uandaaji na utekelezaji wa mipango ya kitaifa na kijamii ya kukabiliana na kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi.
  3. Kuratibu vikao na utekelezaji wa maagizo ya Kamati za Mabadiliko ya Tabianchi.
  4. Kukusanya na kuweka kumbukumbu zinazohusiana na maeneo yanayoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.
  5. Kuratibu utekelezaji wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika taasisi mbalimbali.
  6. Kushirikiana na sehemu ya Elimu ya Mazingira katika kuhamasisha jamii juu ya masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Sehemu ya Mipango, Sera na Utafiti .

  1. Kuandaa na kuratibu utekelezaji wa programu, mikakati, mipango na miongozo ya usimamizi na uhifadhi ya mazingira.
  2. Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Mazingira, Sheria ya Mazingira.
  3. Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa miongozo ya Mkakati wa Tathminini ya Kimazingira (SEA).
  4. Kupendekeza viwango vya mazingira.
  5. Kuratibu utekelezaji wa Mikataba ya Mazingira ya Kimataifa.
  6. Kufanya utafiti wa mazingira.

Sehemu ya Elimu ya Mazingira.

  1. Kubuni na kutayarisha program, mikakati na mipango ya kuelimisha na kushajihisha jamii juu ya kulinda na kuhifadhi Mazingira.
  2. Kushirikiana na Wizara ya Elimu katika uandaaji wa Mitaala ya somo la Mazingira kwa Skuli za Msingi, Kati na Sekondari;
  3. Kuratibu usimamizi wa Maktaba pamoja na kuweka takwimu za Idara;
  4. Kuratibu na kuunganisha vitengo vyote vya Idara katika masuala ya habari na mawasiliano;
  5. Kuandaa programu za maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani pamoja na maadhimisho mengine yanayoambatana na uhifadhi na usimamizi wa Mazingira;
  6. Kuandaa na kuchapisha Taarifa ya Hali ya Mazingira Zanzibar kila kipindi cha miaka mitano.
  7. Kuandaa machapisho mbalimbali ya kimazingira.

Sehemu ya Hifadhi ya Bioanuwai:

  1. Kusimamia na kuratibu uhifadhi wa bioanuwai/maliasili za nchi kavu na baharini;
  2. Kuhifadhi na kuweka matumizi endelevu ya bioanuai/maliasili kwa ajili ya matumizi ya sasa na baadae;
  3. Kuandaa miongozo na taratibu za usimamizi, uhifadhi na uendelezaji wa bioanuwai;
  4. Kushajihisha Jamii juu ya matumizi bora na uhifadhi wa maliasili/bioanuwai;
  5. Kuratibu shughuli za uendelezaji na usimamizi wa rasilimali za ukanda wa pwani (ICZM);
  6. Kufanya ufuatiliaji na tathmini za shughuli zinazohusiana na maliasili/bioanuwai pamoja na mazingira yake.

Sehemu ya Utawala na Fedha.

  1. Kusimamia shughuli zote za Kiutawala, Uendeshaji na Rasilimali Watu za Idara;
  2. Kusimamia mipango ya matumizi na manunuzi ya Idara;
  3. Kuratibu na kusimamia mpango wa mafunzo kwa watumishi wa Idara;
  4. Kusimamia mambo mtambuka kama vile UKIMWI, Jinsia, Ulemavu n.k
  5. Kutayarisha ripoti za matumizi ya fedha ya Idara kwa robo, nusu na mwaka.
  6. Kuandaa na kusimamia MTEF wa Idara.

Ofisi ya Mazingira - Pemba:

Ofisi hii ina majukumu ya kuratibu, kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa kazi zote za Idara ya Mazingira kwa upande Pemba. Aidha, Ofisi hii ina jukumu la kumshauri Mkurugenzi wa Mazingira juu ya utekelezaji wa kazi Idara ya Mazingira katika kisiwa cha Pemba.

MAFANIKIO YA IDARA YA MAZINGIRA

Idara ya Mazingira imefanikiwa kutayarisha nyenzo za usimamizi wa mazingira ikiwemo;

  1. Sera ya Mazingira 2013
  2. Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2015
  3. Muongozo wa Mkakati wa Tathmini ya Usimamizi wa Mazingira 2020
  4. Muongozo wa Tathmini ya Athari ya Mazingira 2020
  5. Kanuni ya Marufuku ya Mifuko ya Plastiki 2018
  6. Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi 2014
  7. Kanuni ya Tathmini ya Athari za Kimazingira 2019
  8. Kanuni ya Uangamizaji wa vitu visivyofaa kwa matumizi ya mwaka 2019.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz